Zungu ataka huduma njia za internet zichangie pato la Taifa

Naibu Spika, Mussa Hazzan Zungu

Muktasari:

  • Naibu Spika, Mussa Hazzan Zungu ameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuzifanya huduma za njia za ‘internet’ (internet gateway) zichangie pato la Taifa (GDP).


Dodoma. Naibu Spika, Mussa Hazzan Zungu ameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuzifanya huduma za njia za ‘internet’ (internet gateway) zichangie pato la Taifa (GDP).

Zungu amesema hayo kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi kuhusiana na hoja zake alizozitoa bungeni wiki hii.

Miongoni mwa hoja hizo ni mapato yaliyoko kwenye umiliki wa njia za kutoa huduma ya internet (internet gateway), lakini siyo kwa kutoza bando.

“La pili, Tanzania hatuna GDP kwenye internet, ‘sovereignty’ ya internet gateway iko nje ya nchi kwa maana hiyo pesa zinakwenda nje ya nchi tunapowasiliana kwa kutumia internet. Sisi tunao ‘service providers’ (watoa huduma), lakini na wao vile vile wanalipa hizi pesa nje ya nchi.

“Nikuombe mheshimiwa Nape (Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye), wewe ni mtaalamu na wewe ndio mwokozi wa nchi hii tunakutegema wewe hufanye haya mabadiliko nchini mwetu tupate pesa nyingi kwenye intarnet.

“Sasa hivi mapato mengi ya simu siyo kwenye kupiga simu ni kwenye data, huko ndiko fedha zilipo. Kwa hiyo nakuomba wewe na wizara yako wa kushirikiana na Wizara ya Fedha, muweke mkakati maalumu wa kuhakikisha ‘gateway internet’ (njia ya internet inabaki nchini na mapato haya yabaki nchini tusilipe nje ya nchi.

“Internet inaweza ikawa sehemu moja ya maeneo mengi nchini hata vijana hawa wakawa ‘service providers’ (watoa huduma, najua siyo jambo dogo litapigwa vita sababu ni suala la pesa, hapa tunazungumzia masilahi ya Taifa, kumsaidia Rais (Rais Samia Suluhu Hassan) apate mapato, kusaidia vijana wapate ajira kuwa watoa huduma kwenye internet,” alisema.

Fuatilia mahojiano kamili kwenye gazeti la Mwananchi kesho Jumamosi ya Septemba 24, 2022.