Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Lenacapavir’ dawa iliyoonyesha ufanisi kuzuia VVU kwa asilimia 100

Muktasari:

  • Ni dawa ya sindano aina ya lenacapavir inayotolewa kwa kundi la wasichana na wanawake mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya VVU.

Dar es Salaam. Dawa ya sindano aina ya lenacapavir inayozuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi, imeonyesha ufanisi kwa asilimia 100 katika jaribio la kwanza la utafiti nchini Uganda.

Iwapo lenacapavir itaidhinishwa, inaweza kubadili kabisa mikakati ya kuzuia VVU duniani.

Lengo la utafiti huo lilikuwa ni kutafuta suluhu ya changamoto katika matumizi, ufuasi na kudumu katika matumizi ya dawa za kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi (PrEP) miongoni mwa wanawake.

Utafiti huo ulioongozwa na mwanasayansi kutoka nchini humo anayefanya kazi katika shirika la Gilead Sciences, Alexander Kintu, umeonyesha utasaidia kupunguza maambukizi kwa wasichana balehe na wanawake vijana katika maeneo yenye hatari kubwa kama Afrika Kusini na Uganda.

Kwa mujibu wa Kintu, walifanya utafiti wa kliniki wa awamu ya tatu, bila kujulikana nani anapokea dawa halisi, na uliodhibitiwa, kwa kushirikisha wasichana balehe na wanawake vijana kutoka Afrika Kusini na Uganda.

“Tuliwagawa washiriki kwa makundi kupokea sindano ya lenacapavir kila baada ya wiki 26, tembe za kila siku za emtricitabine-tenofovir alafenamide (F/TAF), au tembe za kila siku za emtricitabine-tenofovir disoproxil fumarate (F/TDF) kama dawa ya kulinganisha.

“Wote pia walipokea dawa ya bandia kwa njia tofauti na waliyopewa dawa halisi,” amesema.

Kintu amesema miongoni mwa washiriki 5,338 waliokuwa hawajaambukizwa VVU mwanzoni, kulikuwa na maambukizi 55.

“Hakuna maambukizi kwa washiriki 2,134 waliopokea lenacapavir, maambukizi 39 kwa washiriki 2,136 waliopokea F/TAF na maambukizi 16 kwa washiriki 1,068 waliopokea F/TDF.

“Kiwango cha maambukizi ya VVU katika idadi ya watu waliopimwa awali 8,094 kilikuwa 2.41 kwa kila watu 100 kwa mwaka,” amesema Kintu.

Amesema maambukizi ya VVU hayakupatikana kabisa kwa waliopokea lenacapavir, ukilinganishwa na kiwango cha kawaida cha maambukizi, na pia ulikuwa chini ikilinganishwa na F/TDF.

Kwa upande wa F/TAF, haikuonyesha tofauti kubwa na kiwango cha kawaida cha maambukizi na hakuna tofauti ya maana kati ya F/TAF na F/TDF.

Kintu amesema ufuasi katika kutumia tembe za F/TAF na F/TDF ulikuwa wa chini. Hakukuwa na matatizo ya kiafya yaliyojitokeza. Reactions za sehemu ya sindano zilikuwa nyingi zaidi kwa waliopokea lenacapavir (asilimia 68.8) ukilinganisha na waliopokea sindano ya bandia kwa asilimia 34.9.

Amesema washiriki wanne tu sawa na asilimia 0.2 wa lenacapavir walilazimika kuacha kutumia dawa kwa sababu ya maumivu au matatizo ya sindano.

“Hakuna mshiriki hata mmoja aliyepokea sindano ya lenacapavir mara mbili kwa mwaka aliyepata maambukizi ya VVU. Kiwango cha maambukizi kwa kundi hili kilikuwa cha chini mno, kikilinganishwa na kiwango cha kawaida na pia kikilinganishwa na F/TDF,” amesema Kintu.

Kazi ya Kintu ina umuhimu wa kibinafsi kwa kuwa wakati wa kilele cha janga la VVU nchini Uganda, alishuhudia athari mbaya za virusi hivyo kwa familia nyingi, ikiwa ni pamoja na familia yake mwenyewe.

Tukio hilo la awali ndilo linalochochea dhamira yake ya kuendeleza mbinu bunifu za kinga kwa watu wanaotengwa na kukosa huduma bora.

Akiwa na shahada ya uzamivu (PhD) kutoka Harvard na tuzo kadhaa za utafiti kutoka Gilead, Kintu ni mfano halisi wa ushawishi unaoongezeka wa Uganda katika utafiti wa kimataifa wa biomedicine.