Jinsi ya kuepuka shinikizo la damu

Wagonjwa wa kisukari wanaweza kupata magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la moyo ikiwa watakuwa na mitindo mibaya ya maisha pamoja na lishe isiyo na mpangilio.

Shinikizo la moyo kusababishwa na ukosefu wa damu inayokwenda kwenye moyo. Mara nyingi hutokea kutokana na kuziba kwa mishipa ya moyo au ateri, hivyo kusababisha damu kutofika kwenye moyo.

Hali hii husababisha maumivu ya kifua, wakati mwingine shinikizo la moyo hutokea bila kupata maumivu ya aina yoyote. Shinikizo hili huitwa shinikizo tulivu la moyo.

Pia mapigo ya moyo kwenda haraka, kutokuona vizuri, pamoja na damu kutoka puani.

Endapo mgonjwa atashindwa kudhibiti hali ya shinikizo la damu, anaweza kupata madhara kama kuziba kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo, shambulio la moyo (heart attack), mishtuko midogo midogo au mikubwa inayosababisha kuzimia, ugonjwa wa kibofu cha mkojo, kiharusi, kupungua kwa nguvu za kiume, kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama kupoteza kumbukumbu.

Ili kuepuka maradhi hayo, mgonjwa wa kisukari anatakiwa kutumia dawa na kufuata masharti ya chakula na lishe pamoja na mazoezi.

Kwa wasio na ugonjwa wa kisukari wanaweza kujikinga kwa kubadili mfumo wa maisha kama kuacha ulevi, uvutaji sigara, ulaji hasa wa vyakula vya mazao ya mimea kuliko wanyama.

Pia kula vyakula kama nafaka, vyakula vya mbegu, mboga za majani na matunda yenye nyuzi nyuzi kama machungwa. Pia acha kutumia vyakula vyenye chumvi nyingi na sukari pamoja na vyakula vilivyosindikwa viwandani kama nyama za makopo.

Ni muhimu pia kufanya vipimo vya moyo mara kwa mara ili kugundua mapema una tatizo hilo.

Mwandishi wa makala hii, Lucy Johnbosco ni mshauri wa wagonjwa wa kisukari.