Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukila karoti utapata faida hizi

Muktasari:

  • Mtaalamu wa masuala ya lishe kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Scholastica Mlinda anasema karoti husaidia kuondoa sumu mwili na kuongeza kinga ya mwili

Virutubisho vingi tunavipata katika matunda, mboga za majani, samaki, nyama na vyakula vingine huku tukitumia karoti kama kiungo kwenye mapishi.

Licha ya karoti kuzuia maradhi yanayosababishwa na kasoro ya ugawanyikaji wa seli mwilini, bado jamii haijui thamani yake katika ulaji unaofaa, badala yake imeishia kuwa kiungo.

Mtaalamu wa masuala ya lishe kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Scholastica Mlinda anasema karoti husaidia kuondoa sumu mwili na kuongeza kinga ya mwili.

Anasema ina vitamini inayosaidia kusafirisha mafuta mwilini, huboresha ngozi ya mtumiaji na uwezo wa kuona.

Karoti ni chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zenye virutubisho ambazo husaidia katika umeng’enyaji wa chakula na pia mlaji hupata haja kubwa kwa urahisi.

Vile vile tunda hili hulikinga tumbo na magonjwa mbalimbali ikiwamo saratani ya utumbo na huimarisha afya ya kinywa.

Pia, huimarisha fizi na kuzilinda zisishambuliwe na magonjwa ya kinywa na kukiacha kinywa kikiwa na harufu nzuri.

Karoti unaweza kuitumia kutengeneza juisi , saladi kwa kuchanganya na matunda au kachumbari.

Mbali na faida hizo, Mlinda anasema karoti inapokuwa mwilini husaidia kusaga sumu zilizopo katika ini na kuzisafisha katika kibofu na utumbo mkubwa ili ziweze kutolewa nje kwa njia ya haja ndogo au kubwa.

Pia, husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa kuwa carotenoids iliyopo ndani ya karoti husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu.

Kutokana na faida hizi, Mlinda anasema ni wajibu kutumia karoti katika kila mlo ili kuupa mwili ngumu na kuepuka kupata magonjwa ya kinywa na saratani ya utumbo mpana.

Madhara

Mlinda anabainisha kuwa vitamini A, inayopatikana katika Karoti, ikizidi mwilini inaweza kuleta madhara katika mwili, hasa watoto wadogo.

Miongoni mwa madhara hayo kwa watoto ni kubadilisha rangi ya mwili na kuwa na rangi kama ya karoti hasa katika sehemu za miguu na mikono na matatizo hayo huonekana zaidi kwa watoto.

Makala haya yameandikwa na mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Hadija Jumanne