Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukweli wanaume kuugua UTI



Maambukizi kwa njia ya mkojo, kwa kitabibu hujulikana kama Urinary Track infections (UTI). Inakadiriwa mwanaume mmoja kati ya wanaume 100 amewahi kupata tatizo hili nyakati fulani.

Ni maambukizi yanayohusisha mfumo wa mkojo yaani figo, mirija inayoleta mkojo katika kibofu, kibofu cha mkojo na mrija wa kutolea mkojo nje ya mwili.

Vijidudu vinavyochangia maambukizi ya tatizo hili huwa ni bakteria, fangasi na mara chache sana virusi.

Mara nyingi wanaume wamekuwa wakipata hofu juu ya tatizo hili; baaadhi hudhania kuwa tatizo hili moja kwa moja linahusiana na magonjwa ya yanayoenea kwa njia ya kujamiana.

Baadhi ya magonjwa yatokanayo na kujamiana bila kinga yanaweza kuwa na dalili kama zile za UTI, ikiwamo kuhisi maumivu au kuungua wakati wa kukojoa.

Lakini kama ni magonjwa yanayoenea kwa kujamiana Kiingereza maarufu kwa jina la ‘Sexually Transmitted Infections (STI), huwa na dalili ya ziada ikiwamo kutokwa uchafu kama usaha au maji meupe kama maziwa katika njia ya mkojo.


UTI kwa wanaume

Tatizo la UTI ni mara chache sana kuwapata wanaume katika maisha yao, mara nyingi huwa ni wanaume wenye miaka 50 kuendelea. Hii ni kwa sababu ya matatizo ya tezi dume yanayoweza kukabili watu wa kundi hilo.

Huwapata watoto wadogo, vijana na watu wazima ambao huwa ni kwa sababu ya matatizo ya kimaumbile. Hoja ya wanaume kutojali usafi kimwili bado haichangii kwa kiasi kikubwa tatizo hili.

Wanawake wanapata tatizo hili kwa kiwango kikubwa kutokana na maumbile yao ikiwamo uke kuwa karibu na njia ya haja kubwa hivyo kurahisisha bakteria waliopo njia hiyo kusababisha tatizo hili.

Bakteria hao hujulikana kitabibu kama E.Coli. Hawa wakiwa njia ya haja kubwa hawana athari, ila wanapohama eneo jingine la mwili husababisha maambukizi.

Kwa kawaida wanaume hawapati sana UTI kutokana na kuwa na maumbile tofauti ikiwamo kuwa na mrija mrefu wa kutolea mkojo kuliko kinamama jambo ambalo ni faida kwao.


Wanaume walio hatarini

Wanaume walio katika hatari ya kupata UTI ni wenye miaka zaidi ya 50, wenye tatizo la kuvimba tezi dume, kisukari, mawe katika figo au kibofu na upungufu wa kinga mwilini, wasiotahiriwa na wenye kuwekewa mrija wa mkojo.

Dalili anazopata mwanamke ni sawa na zile anazopata mwanaume, waathirika wa tatizo hili au wanaodhani wana tatizo hilo hufika katika huduma za afya wakishitakia dalili mbalimbali ikiwamo mkojo kuwa na harufu kali na uhitaji wa kwenda haja mara tu baada ya kukojoa.

Vile vile mkojo kuwa na rangi nyeupe,  kijivu wenye kiwingu, maumivu wakati wa kukojoa, kuhisi kuungua wakati wa kukojoa na kwenda haja  mara kwa mara, uwepo wa damu katika mkojo,  maumivu ya kiuno na  mgongo.

Wanaume wanaopogundulika kuwa na UTI hushauriwa kuchunguza matatizo mengine ikiwamo uwepo wa mawe katika figo, kuvimba tezi dume na tatizo la mkojo kurudi nyuma katika figo.

Uwepo wa harufu kali ya mkojo si mara zote ni UTI, inawezekana sababu ni aina ya vyakula unavyokula. Jaribu kujichunguza pale unapokula nyama ya mbuzi utaona mabadiliko ya harufu ya mkojo.

Pia unywaji wa pombe, kuugua ugonjwa wa kisukari na kutumia dawa ikiwamo antibiotic, kunaweza kusababisha mkojo kuwa na harufu tofauti inayoweza kukustua.

Mara nyingine mabadiliko ya rangi na harufu ya mkojo yanaweza kuchangiwa na uwepo wa upungufu wa maji mwilini au kutokunywa maji mengi.

Hivyo si kila viashiria kama hivi ni dalili za UTI, kwa wanaume ni vizuri kufika katika huduma za afya pale unapoona dalili zilizotajwa hapo juu.