Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watumiaji ‘energy drinks’ waja na mapya

Muktasari:

  • Uchunguzi wa Mwananchi umebaini baadhi ya watumiaji hasa vijana wanatumia vinywaji hivyo,  kwa kuchanganya na dawa za kutuliza maumivu kwa lengo la….

Dar es Salaam. Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa kukiibuka dhana ambazo hazijathibitishwa kitaalamu,  juu ya matumizi ya dawa na vinywaji mbalimbali kwa lengo la kuongeza nguvu za kiume hasa kwa vijana.

 Miongoni mwa dhana hizo potofu ni kuchanganya  dawa za kutuliza maumivu pamoja na vinywaji vya kuongeza nguvu maarufu "energy drinks."

 Baadhi yao huamini kuwa mchanganyiko wa hivi viwili,  unaweza kuongeza stamina au uwezo wa kufanya tendo la ndoa.

 Hata hivyo,  kwa mujibu wa wataalamu na ripoti mbalimbali za afya,  matumizi ya mchanganyiko huo si tu hayana msingi wa kisayansi, bali yanaweza kuwa na madhara makubwa kiafya.

 Ally Ally Mkazi wa Tabata anasema amekuwa akisikia kuwa matumizi ya mchanganyiko,  hutumika kusaidia kuongeza nguvu za kiume.

 “Baadhi ya vijana wamekuwa wakitumia kama mbadala wa ‘busta’ kwa ajili ya kuongeza  stamina wakati wa tendo, ”anasema.


John Mpogole (si jina halisi) mkazi wa Temeke anasema matumizi ya mchanganyiko huo ulimsababishia kupata changamoto ya uraibu,  hivyo kushindwa kufanya tendo la ndoa bila ya kutumia mchanganyiko huo.

 “Hali hiyo ilinitesa kwa muda wa miezi kadhaa hadi pale nilipopata msaada wa kitaalamu, ”anaeleza.


Kauli za wataalamu

 Akizungumza na Mwananchi,  mtaalamu wa lishe kutoka Shirika la Word Vision, Dk Daudi Gambo anasema hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa matumizi ya mchanganyiko huo,  unasaidia kuongeza nguvu za kiume, badala yake unaweza kuleta madhara katika ini, figo pamoja na moyo.


Anasema dawa hizo za maumivu zilitengenezwa kwa ajili ya kutuliza maumivu na kushusha homa, na wala  hazikutengenezwa kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume.

 Anaasema matumizi ya dawa hizo kwa njia isiyo sahihi, kama kuchanganya na energy drinks au kutumia bila sababu ya kiafya au kushauriwa na daktari , yanaweza kuathiri ini na figo na kuzifanya kushindwa kufanya kazi vizuri.

 “Ini  ni moja ni kiungo cha lazima katika mwili wa binadamu ili kuwezesha maisha ambapo kazi yake kubwa ni kama chujio ambalo huchuja damu inayozunguka mwilini, ”anasema na kuongeza kuwa linaposhindwa kufanya kazi vizuri, sumu mbalimbali zinazoingia mwilini kwa njia ya chakula au vinywaji zitashindwa kuchujwa vizuri na kubaki mwilini jambo ambalo ni hatari kwa afya.

Kwa upande wa figo anasema: “Figo inaposhindwa kufanya kazi vizuri,  husababisha mwili kuwa na mrundikano wa maji yaliyozidi ambayo yangelihitaji kutolewa kwa njia ya mkojo”

 Anaongeza: “Pia huweza kusababisha takasumu na mabaki mengine yasiyohitajika mwilini kurundikana hali inayoweza kuleta changamoto mbalimbali katika mwili.’’

Anaeleza kuwa mbali ya athari hizo za kiafya,  matumizi ya mchanganyiko huo, yanaweza kuwafanya wahusika kuwa waraibu na hivyo kushindwa kuwajibikaa vilivyo kwenye tendo la ndoa pasipo kutumia mchanganyiko huo.

 Anasisitiza kuwa matumizi ya dawa za maumivu na energy drinks kwa lengo la kuongeza nguvu za kiume,  ni jambo lisilo sahihi na lenye madhara makubwa kiafya,  hivyo anawataka vijana kupuuza dhana hizo potofu.

 “Afya njema huanza na kuwa na maarifa sahihi, epuka matumizi ya dawa au vinywaji visivyo na ushahidi wa kitaalamu kufanya kazi fulani katika mwili”anasema.

 Kwa upande wake, Daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi, Dk Isaya Mhando anawataka vijana kuacha kuamini kila wanachokiona mtandaoni hasa kinachohusu afya hasa ikiwa hakijathibitishwa kisayansi.

 Anawasihi vijana kuachana na dhana hizo na kujikita kuishi kwa mitindo mizuri ya maisha ili kuwa na afya bora.

 Anawahimiza kuzingatia lishe bora, ufanyaji wa mazoezi, kuepuka matumizi ya pombe na sigara kupita kiasi na kuepuka msongo wa mawazo ili kuimarisha afya zao.

 “Ni muhimu kwa mtu yeyote mwenye changamoto hizi kutafuta msaada sahihi wa kitaalamu,  badala ya kujihatarisha kwa kutumia dawa au vinywaji visivyofaa, ”anasisitiza.