Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Charles Baba adai amerudi kwenye dini ya mama yake

Muktasari:

  • Kubadili diniMwimbaji huyo wa kundi la Twanga Pepeta ameb-adili dini na kuingia Uislamu na sasa anaitwa Abdulmalik.

Wiki iliyopita mwanamuziki Charles Baba alifunga ndoa na Mariam Shabani, huku gumzo likiwa ni mkali huyo wa dansi kubadili dini na kufuata ya mkewe.

Akizungumza na Mwananchi amesema anajua imewashangaza wengi, lakini ukweli ni kwamba amerudi katika dini ya mama yake anayeitwa Asha Ramadhani, hivyo hakuna kilichoharibika na sasa anapenda afahamike kwa jina la Abdulmalik.

Charles Baba ambaye ni muimbaji katika bendi ya Twanga Pepeta kwa sasa, anakiri kwamba watu wamekuwa wakijiuliza kwa nini kabadili dini ukizingatia kuwa ndoa yake ya kwanza alifunga kanisani.

“Naomba leo niwatobolee siri sababu ya kubadili dini, mbali na kwamba nimeamua kuwa sawa na mke wangu, pia nimerudi katika dini ya mama yangu.Nadhani mtakuwa mmenielewa hivyo hakuna kilichoharibika,” amesema.

Kuhusu kudaiwa kafuata fedha

Amesema anawashangaa wanaomtuhumu kwa hilo kwani hata vitabu vya Mungu vinasema unapaswa kuoa mwanamke mwenye uwezo hivyo kama ndivyo wanavyodhani basi atakuwa hajatenda kosa. “Mtume wetu Mohamed (S.A.W), alimuoa Bi Hadija ambaye alikuwa mmoja wa wanawake matajiri, hivyo na mimi sijafanya kosa, kikubwa tu isiwe ndio nibweteke kama mwanaume katika kuendelea kutafuta riziki ya kumuhudumia mke wangu vile ninavyojaliwa.

Kuhusu sakata la kuwa na ndoa ya Kikristu kabla ya hiyo, alikiri kuwa lina ukweli na kueleza kuwa mwanamke huyo walishindwana na kila mtu akawa na maisha yake, kama kijana dini inakataza zinaa ndio maana kaamua kuoa tena.

Akimuelezea mke wake Mariam, amesema ni mtu ambaye wamejuana muda mrefu kabla ya mke aliyemuacha, na anashukuru pamoja na yote yaliyotokea lakini amekubali kurudiana naye na hatimaye kuoana.

“Kwa kweli alichonifanyia mke wangu ni mapenzi yaliyopitiliza, namshukuru pamoja na milima na mabonde tuliyopitia ameamua kunikubalia niwe mume wake, naahidi sitomuangusha katika maisha yetu haya mapya ya ndoa,” amesema.