Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PASTOR MYAMBA: Chuo changu kitaondoa kero ya maadili kwenye sanaa

Mwigizaji,Emmanuel Myamba.

Muktasari:

“Ninavyoishi kwenye filamu ndivyo ninavyoishi nje ya filamu,” anasema.
Msanii huyu maarufu kwa jina la Pastor Myamba, anasema kuwa yeye ni Mkristo safi na ameokoka, akiongeza kuwa ni muumini wa Kanisa la Living Water.

WAIGIZAJI wengi huishi tofauti na jinsi tunavyowaona katika filamu na michezo mbalimbali ya luninga.

Lakini kwa Emauel Myamba, hali ni tofauti kwani kwa maneno yake anasema kuwa maisha yake hayana tofauti.

“Ninavyoishi kwenye filamu ndivyo ninavyoishi nje ya filamu,” anasema.
Msanii huyu maarufu kwa jina la Pastor Myamba, anasema kuwa yeye ni Mkristo safi na ameokoka, akiongeza kuwa ni muumini wa Kanisa la Living Water.
Mnyamba ametokea kuwa kipenzi cha Watanzania wengi kutokana na aina yake ya uigizaji kama mchungaji.
Myamba,  ambaye hadi sasa ameshacheza filamu 38, anasema kuwa fani hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi hata yeye kuamua kufanya shughuli nyingine za ujasiriamali.

Msanii huyo anayemiliki kampuni mbili tofauti nchini, Januari mwaka huu alifungua chuo cha kufundisha taaluma ya uigizaji kwa lengo la kukuza vipaji hapa nchini.
Chuo hicho kinachofahamika kwa jina la ‘Tanzania Film Training Center (TFTC)  kipo maeneo ya Ubungo, jijini Dar es Salaam kikiwa na wanafunzi 200 hadi sasa.
Anasema kuwa chuo chake kinatoa mafunzo mbalimbali, ikiwemo kozi nne muhimu ambazo ni  kuigiza, kupiga picha, kuandika na maadili katika uigizaji.
Kwa mujibu wa Myamba, ameamua kuanzisha chuo hicho ili kulinda maadili katika sanaa ya uigizaji nchini, ambayo alisema yanayumba kwa kaisi fulani.

“Mbali na chuo hicho pia nimezindua gazeti maalumu kwa ajili ya habari za filamu na sanaa za maigizo tu na sababu kubwa ni kuhakikisha ninawatangaza wasanii chipukizi wa filamu,” anasema na kuongeza:
“Lakini pia, gazeti hili litakuwa mahususi kwa ajili ya kuandika mambo yet mazuri.”
 Anasema kuwa baadhi ya magazeti nchini hasa yanayoitwa ‘magazeti pendwa’ yamekuwa yakiandika habari mbaya zisizokuwa na ushahidi kwa ajili ya kufanya biashara zao, hivyo kupitia gazeti hilo, anasema wasanii hawatakuwa na haja ya kuangaika na magazeti kama hayo.

“Magazeti yao sijui kama yanafuata taaluma, maana unaposikia habari za msanii ninavyojua ni lazima umfuate kwanza anayetuhumiwa kabla ya kuandika. Lakini wao wanaandika tu ndiyo sababu ya kuchukiwa, kwa sehemu kubwa sana yana hali upotoshaji, ”anasema Myamba.
Kuanza sanaa

“Kwa mara ya kwanza mimi kuanza sanaa hii nilichukuliwa na Marehemu Steven Kanumba, wakati tukiwa Shule ya Sekondari Jitegemee, kidato cha sita. Kanumba alinichukua na filamu ya kwanza kuigiza naye ilikuwa ni Johari sehemu ya kwanza na ya pili,” Myamba anaelezea jinsi aivyoingia kwenye uigizaji wa filamu.

Anasema  kuwa baada ya kumaliza kidato cha sita, aliendelea na masomo ya chuo kikuu huku akiwa tayari ameshatambulishwa rasmi kwenye sanaa na kuongeza kuwa, aliendelea kucheza filamu ingawa siyo kwa kasi kubwa, hadi alipomaliza chuo mwaka 2009 na kufungua kampuni ya filamu inayojulikana kama  ‘Born Again Films.’
Anasema kuwa kupitia kampuni hiyo, ameshacheza filamu 10 na filamu iliyompatia kipato kikubwa kuliko filamu zingine ni ya  ‘Pastor Myamba Trial’.
Hata hivyo hakuwa tayari kueleza kiasi cha fedha alichoingiza kupitia filamu hiyo.

Mafanikio yake
Myamba anasema kuwa kupitia sanaa, sasa anaweza kuishi maisha mazuri na anajiandaa kuitengenezea familia yake mazingira mazuri ya kuishi bila shida.

“Nina kiwanja eneo la Madale, ninajenga kwa ajili ya familia yangu. Nategemea mwakani nitakuwa na familia, chuo changu na gazeti hili vinalipa kwa sehemu kubwa sana na upande wa sanaa siyo mbaya, mkate wa kila siku unapatikana,”anasema na kuongeza:

“Mkate wa kila siku unapatikana bwana, lakini wezi wa kazi zetu ndiyo wanazidi kuongezeka na juhudi za kupambana nao ni kidogo sana.”
Anatoa wito wa kuendelezwa kwa juhudi za kupambana na wezi wa kazi za wasanii ili kazi hizo zinufaishe wasanii.

Mahusiano
Kuhusu mahusiano anasema: “Ninaye mchumba na sipendi kumweka wazi, ila wakati utakapofika Watanzania watamwona. Familia yangu ina ushirikiano wa karibu sana na mimi, ”anasema Myamba na kuongeza:

“Kwa bahati mbaya sana pamoja na kuwa sijaoa, napambana na vishawishi vya ngono. Kwangu ni mwiko kutembea na mwanafunzi wangu, hata kama nikitambua kuwa mwalimu wangu amefanya hivyo, sheria inaniruhusu kumuadhibu kimaadili.”
Myamba anasema kuwa suala la kuchanganya mapenzi na kazi ni kasoro iliyochangia watu wengi kuanguka katika harakati zao za kutafuta maisha.