Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unayopaswa kufikiria kabla ya kuingia kwenye ndoa



Canada. Japo tumewahi kugusia kwa mbali na, kwa ufupi kudurusu, kujadili masuala yafuatayo kuhusiana na ndoa hasa mambo muhimu kudurusu na kujua kabla ya kuamua kufunga ndoa hatukuyajadili kwa undani.

Sasa tunarejerea, Tunafanya hivyo kwa kujua wazi kuwa hatukuzama sana. Isitoshe, binadamu ni kiumbe anayesahau kirahisi. Hivyo, leo tutadurusu baadhi ya mambo ambayo hatujawahi kuyagusia kwa undani na upekee kuhisiana na ndoa hasa kwa wanandoa ambao wanatarajiwa au hawajingia kuingia kwenye ndoa. Haya mambo ni ya kawaida  ila muhimu sana. Hivyo, ni bahati mbaya na kawaida kutoyazingatia kutokana na sababu mbali mbali ziwe za bahati mbaya au makusudi.

Tuanze na dini. Japo hatupendi kuingilia mambo ya dini japo nayo yanaingilia mambo ya wengine, tukiri. Katika maisha hasa ya ndoa, huwa hapakosi migawanyiko, ubaguzi wa kidini au udini na mengine kama hayo.

Dini ni suala mtu binafsi tena nyeti na tata kwa jamii zilizopokea dini za kimapokeo, ambazo zimetugawanya sana japo tunajitahidi kuficha kana kwamba kila kitu ni shwari.

Mosi, dini zote za kimapokeo zinachukiana na kushindana kutafuta wafuasi ili kujipatia kipato na uhalali. Hivyo, kwa waliozipokea, hujikuta wakiwa waathirika hata kwa mambo ambayo si hawajui tu bali hata hayawafai. Ndoa pia haiepuki mambo haya.

Pili, dini husika, licha ya kuzuia au kuweka mazingira magumu kwa wafuasi wake kuoa au kuolewa na wafuasi wa dini pinzani, ni changamoto kubwa tu. Mfano, mkristo au muislam haruhusiwi kumuoa kuoa asiye wa dini yake hadi ambadili dini!

Kwa wanaojua jinsi dini zilivyojikita kwa wahusika, kwa watu wa kawaida wasio wabishi, hili jambo ni gumu japo linawezekana. Kutokana na ugumu na unyeti hata utata wake, tunawashauri watarajiwa waliomo kwenye dini tofauti, kulizingatia hili kwa makini kabla ya kufunga ndoa.

 Tatu, japo binadamu ana uwezo wa kuishi popote akiamua, jiografia ina mchango mkubwa katika kufaniksiah au kutofanikisha hili. Hii maana yake ni kwamba tumejikuta tukizaliwa tulipo bila kupanga wala kuchagua.

Hivyo, kabla ya kuamua kuoa au kuolewa, ni vizuri kujua jiografia ya unapokwenda kuishi kwa wale wanaoungana na wenzao au mwenzio anakotoka. Hii ni kwa sababu jiografia na mazingara yetu, huathiri kwa kiwango kikubwa mila na tabia zetu tunapokuwa kwenye maeneo tofauti.

Chuang na Capellan katika utafiti wao, wanasisitiza kuwa tusidharau au kuisahau jigorafia kwenye ndoa kama sehemu mojawapo ya maisha isiyoepukika. Kwani, ina athari japo fiche, kwenye ndoa.

Hebu fikiria. Mgogo, Mnyanturu, Mrangi,  au Msukuma anajikuta Arusha, Karatu, Lushoto, Manyara au Mbeya kwenye baridi tofauti na kwao kwenye joto. 

Mbali na hiyo, mhusika kazaliwa na kukulia kwenye tambarare na ukame. Ghafla bin vuu, anajikuta kwenye miinuko na milima yenye kijani na vito kila mahali. Vaa viatu vyake, ungekuwa wewe, ungejisikiaje?

Nne, tujue hakuna jambo ambalo linafanyika bila malengo. Ndoa, kadhalika, ina malengo na matarajio ya muda au ya kudumu. Ndoa si jambo wala tarajio la muda bali la kudumu. Unapoamua kuoa au kuolewa, lazima uwe na malengo, matarajio, na ndoto unavyolenga kukamilisha na kutimiza.

Tano, tunaweza kujidanganya na kujisahaulisha ili tufanikishe mambo yetu. Baada ya kujiwekea malengo unayolenga kukamilisha, lazima ujiulize swali moja kuu: Je, haya malengo yangu yanafanana au kwenda na na malengo ya mwenzangu?

Hapa, lazima ujue malengo ya mwenzako ambaye pia anapaswa kujua yako. Ndoa ni safari ya maisha. Lazima wawili wasafiri pamoja kwa ukaribu. Pia, lazima waelekee upande mmoja na kushuka kwenye kituo kimoja.

Sita, kuna suala hili la mila. Hapa, tunamaanisha imani na mambo ambayo yote  madogo na makubwa tuyafanyayo kwa sababu ama tumeyarithi au tumeyaamini kama vile mila za asili na dini za kimapokeo.

Mara nyingi, huwa tunafanya mambo haya bila hata kufikiri wala kujua Japo tunaweza kuvidharau au kuvipuuza vitu hivi, vina mchango mkubwa katika maisha ya ndoa.

  Tumalizie. Yaliyojadiliwa hapa ni muhimu katika maisha ya binadamu kwa sababu ni sehemu yake iwe utambulisho au hisia zake za ndani au psyche kwa kimombo. Hivyo, ukiyapuuza, hayatakupuuza.