Ndani ya boksi: Krismasi hii kama Dullah Makabila, wa vizinga pita huku...

What you need to know:

  • Raha ya kumtokea mrembo awe na aibuaibu. Tena siyo aibu kidogo, bali aibu flan hivi kubwa. Ili mkisimama sehemu basi azuge kuchuma majani. Akate tawi la mti au ua. Namna hiyo bana. Yes!

Raha ya kumtokea mrembo awe na aibuaibu. Tena siyo aibu kidogo, bali aibu flan hivi kubwa. Ili mkisimama sehemu basi azuge kuchuma majani. Akate tawi la mti au ua. Namna hiyo bana. Yes!

Ndio walivyoumbwa. Siyo totozi imekaza uso kama nati za trekta. Ama kakutolea macho kama anakudai pesa za vikoba. Kumbe unamuimbisha ili totozi akuelewe ulichonacho chini ya uvungu wa moyo.

Ukiongea na totozi hata kwa saa tatu na zaidi. Kisheria anatakiwa ainamie chini muda wote. Huku akivunjavunja vidole. Najua kuna wanawake wasio na akili watahoji hiyo ni sheria ya wapi? Utadhani kuna sheria yoyote anayoijua.

Achana naye mwanamke wa hivyo. Hapa tunaongelea totozi zenye akili na adabu za kale. Ambazo zikiongea na kidume hung’ata kucha na kubananisha miguu. Akijibu asikuangalie usoni.

Ndiyo! Ndo pozi za kike hizo tangu na tangu. Hata Hawa alipoongea na ‘Baby Nyoka’ alikuwa katoa mimacho tu. Mpaka akalishwa tunda kindezindezi tu huku akiwa katumbua macho. Angeinamisha uso hata ‘Baby Nyoka’ naye angeona aibu kumpiga fiksi. Pia mtoto wa kike anatakiwa achelewe kutoa jibu ikibidi hata baada ya miezi sita na zaidi ndio aseme akubali au akatae. Uliyemtokea 2015 atoe jibu mwaka huu. Tena iwe siku ya Krismasi au mwaka mpya, kukubali au kakataa.

Kinachoshtua siku hizi ukimtokea msichana. Hata kama ulikuwa unatania yeye anajua kweli na anakubali hapohapo. Yaani ni gusa unase mazee. Na kibaya zaidi muda huohuo anakuweka kwenye wadaiwa wake sugu wa bando, chipsi, bia, pesa za saluni, marejesho ya vikoba, nauli za bodaboda, luku na gesi.

Hakuna mwanamume anayeanzisha uhusiano na demu kwa lengo la kumchezea. Tabia ya mademu wengi ndio chanzo cha kubadilisha lengo la mwanamume. Unaitokea pisi asubuhi, jioni inakupa na wadhifa wa baba wa familia. Khaa! Unafahamu jinsi ya kunasa totozi za namna hii na maeneo yao? Pisi za hivi ambazo ni akili mbovu. Zile za Sinza zipe stori za baa mpyampya au klabu za usiku. Hizo ndio stori wanazotaka. Na utazitafuna mpaka uvimbiwe. Lakini ndani ya Sinza kuna pisi zenye akili kubwa zinazostahili kusitiriwa na ndoa.

Pia kuna zile pisi akili chafu za Ilala, Magomeni au Mwananyamala, wao toa ahadi ya kuwapeleka taarabu, hao utawachoka wewe. Wao wanawaza taarabu na kurushana roho kuliko ndoa na uchumba. Ila wapo wenye akili wanaopaswa kuposwa. Kuna zile nguchiro za kike za ushuani Masaki na Oysterbay. Zile ndio ndorobo kwelikweli, wewe ongea sana viingereza na kulamba lamba lipsi. Na simu zako ziwe za kupigia kutoka US na UK. Wako kama ndezi huchanganyikiwa na utawanasa kama kuku.

Wamezaliwa au wamekulia Masaki. Lakini ni washamba kwa mtu anayeongea Kiingereza. Wakati mitaa ya Mabibo ukipendelea sana Kiingereza wanakuona mwanaume mashauzi huna lolote. Utasikia ‘nipishege’ huko. Lakini huko uswazi pia kuna akili mbovu zaidi. Kama Temeke, Buguruni, Vingunguti, Vituka na Kiwalani. Hao usitoe ahadi kabisa, wewe jitahidi tu kuhudhuria shoo za vigodoro usiku. Wakisikia sehemu kuna kigoma cha Uruguay basi utaopoa mtaa mzima. Yaani ndio mizuka yao na wanakuwa kama vichaa.

Kesho yake utawakuta mtaani, kope bandia zimebanduka upande, wako hoi. Hawakulala na hawajala vizuri, wanapiga miayo huku wanasimuliana jinsi walivyomwaga radhi. Yaani msichana rangi ya nguo ya ndani inajulikana mtaa mzima kwa sababu ya kucheza kigodoro.

Mabibo, Kigogo, Mburahati, Keko, Buza na Tandale. Pisi akili mbovu za mitaa hiyo wakijua unafahamiana na Mondi, Kiba, Babu Tale, Baba Levo, Said Fella au Mwijaku. Kwisha habari yao. Mtaa wote watatamani uwape mimba na malezi ya watoto ni juu yao.

Ubungo, Kimara, Mbezi Kibamba, Kinyerezi, Tabata, Segerea mpaka Goba. Pisi mbovu za huko zinapenda sana zikiambiwa upo karibu na viongozi wa Chadema. Hapo umemaliza kila kitu. Sijui ziliambiwa wanapeleka watu peponi? Madem akili mbovu wa Kinondoni, Kijitonyama na Kariakoo. Wewe jifanye mpiga dili za unga, utawatafuna hadi mifupa. Wao huamini utajiri huja kwa dawa za kulevya tu. Hawana akili ya nje ya boksi zaidi ya hapo. Sijui bwege gani aliwadanganya?

Mbagala, Tandika, Mtoni Mtongani, Kwa Aziz Ally na Sabasaba kwa Mpiri. Hata stafu wa TRA, Uhamiaji au Mambo ya Ndani wanapuuzaa. Kule wewe jifanye bodaboda au konda wa daladala. Utaeleweka fasta. Mitaa hiyo pisi akili mbovu huamini kwamba vijana walioendelea zaidi ni bodaboda na makondakta. Maana si ndio wana visenti vya kila siku.

Ubungo Msewe, Mabibo Makuburi, Mlalakuwa mpaka Kawe Ukwamani. Wakijua unajuana na Mzee wa Upako, Askofu Mwingira, Askofu Kakobe, Askofu Gwajima au Mwamposa. Utapewa ulinzi mpaka na mama mkwe ili usiibwe na wengine. Ndiyo maeneo pekee ambayo wasichana wao, huamini muimba kwaya na mfukuza mapepo ndio mwanaume kamili. Kifupi gia ni moja kwao. Jifanye unakemea mapepo hata kwa ishu ya kisheria. Tegeta, Bunju, Boko, Kurasini, Yombo, Kitunda. Kama ni mganga wa jadi, utamiliki pisi kama vile Mfalme Suleiman. Yaani huko waganga ni wengi kuliko bodaboda na bajaji. Kila kijana ndoto yake ni kuitwa mganga wa kienyeji.

Bila shaka wale wenye hofu ya vizinga vya Krismasi, mtakuwa mmeelewa aina ya pisi na maeneo yao. Ukiona vizinga vimezidi mwambie manzi wako pita huku. Kama Dullah Makabila tu. Kifupi hii siyo Krismasi ya vizinga, kila mtu kapigika sana.