Ndani ya boksi: ‘Usingo mamazi’ kumbe ni dili? ‘sijapentaa’!
Muktasari:
- Diamond Platinumz. Mfano halisi wa msela mwenye mafanikio makubwa sana. Mbali na mali nyingi alizonazo, pia ana makidi wanne aliopata kwa pisi kali tofauti tofauti. Kaanza Zari, Hamisa kisha Tanasha!
Diamond Platinumz. Mfano halisi wa msela mwenye mafanikio makubwa sana. Mbali na mali nyingi alizonazo, pia ana makidi wanne aliopata kwa pisi kali tofauti tofauti. Kaanza Zari, Hamisa kisha Tanasha!
PESA! Imekataa kumtuliza Mondi na pisi moko. Cha ajabu kuna ‘mabraza’ wanasubiri wawe kama Mondi ndipo waoe. Wanajizeekea bila ndoa kisa pesa, Mondi ana mkwanja lakini na yeye anajizeeka bila ndoa. Dunia!
Kuna watu pesa hufanya wafunge ndoa kila wiki. Na wengine hufanya washindwe kutulia na pisi moja hata kwa kutwa tu. Anaamkia kwa Janeth, anashinda kwa Julieth na kulala kwa Jasmine. Pesa inamfanya awamiliki atakavyo.
Hapa ndipo ilipo tofauti ya Diamond na Bugatti. Hawa ni washikaji lakini wenye mizuka tofauti ya pisi kali za mjini. El Bugatti kafululiza kuoa pisi kali kila uchwao kama kadata. Mondi yeye kazalisha mfululizo kisha kapita hivi.
Hawa ni washikaji wenye mitazamo tofauti. Mizuka na fikra tofauti juu ya hii makitu. Tunawatolea mfano kwa sababu ni mastaa wenye majina na kueleweka kirahisi mishe zao. Pindi ukitaka kutolea mfano vijana kimjini hawa hawakwepeki.
Na zipo pisi zikipata pesa au ajira tu hukimbia ndoa. Yes! Ndio ukweli huu, kuna tatizo la msingi katika jamii yetu. Pesa zinawafanya vijana wachelewe kuoa na kuolewa. Na pesa zinafanya vijana waachike na kuacha kila siku. Tumeamua pesa ituongoze kwa kila kitu mpaka nafsi zetu, na kutuweka mbali na uhalisia. RITA hupokea maombi ya talaka siyo chini ya 500 Bongo nzima. Katika hilo pisi kali ndio ziko ‘fronti’ kinomanoma kutaka talaka. Ni pisi zile zilizopanda vidato, zilizobukua na kupandisha madini kwa ‘hedi’. Zinazovuta ‘salare’ ndefu. Achana na ubishi wa kindezi, cheki mastaa wetu na wale manzi wa mjengoni Dom pale. Wengi laini moja. Pesa na elimu zina uhusiano mzuri na shetani, kama Mayele na nyavu. Inafanya kila kitu kiwe rahisi kama kuoa, kuolewa, kuacha, kuachwa na usaliti wa ndoa.. Kwa nini elimu na mkwanja huzipa nguvu pisi ya kuwaza kuishi kivyao? Zinawatia kiburi mkurabita? Ama ile jeuri mkukuta na ujasiri wa asasi za kiraia pamoja na viwatilishi vya mahaba nitenge? Aliyebuni pesa alaaniwe. Hutaki maagizo wala maelekezo ya bwege kutoka kiumeni. Unavimba mtoto wa kike na hutaki pigo za unyenyekevu. Yes! ‘Dyadya’ unajikuta kama kiongozi mkubwa hivi tena wa nchi. Una kanafasi flani ‘kene’ kaofisi flani mjini. Mabishoo kibao wapo chini yako. Mkwanja unaingiza kwa cheo chako. Na cheo umepewa kwa elimu yako. Sasa unaanza kuhisi ile heshima ya mume, upewe wewe. Iwe ‘vaisi vesa’ kwa sababu tu una pesa, elimu na cheo ofisini kwako. Ndegelesi. Unataka mumeo afuate agizo lako kama wale mabishoo wa ofisini. Na hizi akili huanzia huku kitaa ngazi ya kaya. Wa kike huambiwa soma sana elimu haina talaka. Tafuta pesa yako ‘dyadya’, hawa wanaume wa leo usiwaamini. Utadhani baba zao ndio waliaminika na mama zao. Matakeo yake ni nini? Watoto wa kike hubaki na mtazamo hasi na jinsi ya pili. Hata walioolewa huleta pigo flani hivi za kiushindani kwenye ndoa hizi. Ndoa ina mwezi tu, hajulikani mume ni yupi na mke yupi. Ni mtiti tu kama Sugu na Stara. Kelele kila siku ndani ya nyumba. Na hii kitu huchagizwa na wanaharakati.
Ambao hawamjengi kifikra mtoto wa kike, bali wanamjazia chuki kubwa na jinsi ya pili. Wanamjaza aamini kuwa anaweza kufanya lolote kama mwanaume. Ni kitu kizuri kumuaminisha hivyo. Ila tatizo linakuja pale anapojengwa wa kike kwa kumbomoa yule wa kiume. Makosa ya wanaume mnahamishia kwa mtoto wa kiume. Matokeo yake ni kumtenga wa kiume na dunia ya sasa.
Neno kichwa cha familia linaanza kupigwa vita kwa nguvu sana. Tena na wale ambao hawawezi kamwe kufanya shughuli zao bila kuanza na kuomba dua. Tena wakiwa ‘laivu’ mamilioni ya watu wakitwatazama.
Dua inatoka kwenye vitabu vitakatifu. Ambavyo ndio vinavyoelekeza suala la kichwa cha familia. Ajabu agizo la kichwa cha familia toka kwa vitabu hivyohivyo linapuuzwa na haohao. Tunajenga jamii ya ovyo. Kuna baadhi ya pisi za mjini. Kitendo cha kuongoza kundi flani la watu, hufanya watake kuwa kichwa cha familia. Wakiona haiwezekani, hapo ndipo ibilisi wa kutaka kuishi bila mwenza anawaingia. Mume yeyote anataka awe juu. Mke akitaka awe juu balaa linaanza hapo. Mume (siyo wote) hutafuta pesa ili ahudumie familia. Mke (siyo wote) hutafuta pesa ili aonyeshe anaweza kuishi bila mume. ‘Dyadya’ kama ofisini kuna masela kibao wanakunyenyekea kama bosi. Usitake na msela wako wa mjengoni (mume) aishi kama hao ndezi wako wa ofisini. Jiheshimu! Mpe nafasi ya kifalme msela. Umtii. Haimaanishi uvumilie hata upuuzi wake. Lakini elimu, cheo au kipato kisikupe kiburi cha ibilisi ukaamini unastahili kuwa juu yake. Utakuwa unatumikia shughuli za shetani ndani ya ndoa. Kama mchizi anazingua fasta tafuta msaada. Usisubiri turefushe jina kwa kuongeza nyuma neno marehemu. Kesi za mtu mbili, malizeni wenyewe bila kuwapa faida mabwege bwege wa mjini. Hivyo tuishi! Leo hii mademu wa mjini wanatukuza na ‘kuubrandi’ sana ‘usingo mamazi’. Wameugeuza kama vile ni ushujaa na wanasifu kwa nyimbo na pambio. Yaani ‘nau deizi’ hilo ni dili kama vile ilivyokuwa dili msichana kubaki na bikira. Wanaona ni ‘fasheni’ kuzalishwa na kutelekezwa. Wakati zamani ilikuwa aibu kuzalia ‘homu’ sasa ni mchongo na ‘unatrendi’ kinoma. Ukibisha wewe tazama mtaani kwako kina ‘dyadya’ wangapi wana watoto bila mume.
Hata bila kitaa hesabu mastaa wa kike wanaomiliki ‘makidi’ bila waume. Kisha uliza masela wako wenye dada ‘homu’, wangapi wamezaa bila ndoa. Ndio utajua kwamba hili ni dili kama dili zingine na ndio habari ya ‘tauni’. Nikiwa mkubwa nitakuwa kama yule Mfalme Sule. Nitaoa wake wengi na masuria ya kutosha. Hata shetani akizeeka hugeuka malaika. Hawa wanaoona ‘usingo mamazi’ ni dili, pia wakizeeka wataona umuhimu wa ndoa. Tukiacha hili kwenye akili za watoto wetu tutaacha dunia ya ajabu. Dunia ya wake tupu bila waume. Kumbuka waume tunadedi kifalafala saaana kuliko wao. Na tukiwa hai hawataki kuishi nasi.
‘Usingo mamazi mai fuuti’. Kuzaa bila ama kabla ya ndoa siyo dhambi. Lakini kujisifu na kudhani ni ushujaa kuwa ‘singo mama pia siyo sahihi. Tuishi!