Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo ya kuzingatia katika kuendesha ujasiriamali kwa mafanikio na furaha

Muktasari:

Kazi zako hasa zile ambazo unaona zinakuzidia ama kwa kuwapa wataalamu wakufanyie au kwa kuwapa wafanyakazi walioko chini yako kama unaona wana uwezo wa kufanya hizo kazi.

Baadhi ya wajasiriamali waliofanikiwa wanajiona kama rasilimali adimu hapa duniani.

Hata hivyo, ukweli ni kuwa kama unataka kuwa mjasiriamali wa ukweli huna budi kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo;
a) Kupata kifungua kinywa na mlo wa mchana stahiki, kwani mwili wa binadamu ni kama gari linalohitaji mafuta.

Baadhi ya wajasiriamali hufanya kazi kupita kiasi na hivyo kusahau hata kula, jambo ambalo ni kosa kubwa kwani mbali ya kuharibu mwili, hufanya akili isifanye kazi yake vizuri na hivyo kukaribisha magonjwa yasiyo ya lazima. Vilevile hukunyima fursa ya kukutana na wateja na marafiki zako wanaotenga muda fulani kwa ajili ya chakula cha mchana ambao huutumia kubadilishana mawazo.

b) Kuwa na ratiba ya kazi za kila siku yenye kutekelezeka kulingana na mahitaji ya shughuli unazozifanya, ambapo jambo la kwanza unalotakiwa kufanya kila siku asubuhi ni kuangalia kalenda yako na kuweka vipaumbele vya kazi zinazotakiwa kufanywa kwa siku hiyo.

c) Usijihusishe na usomaji wa barua pepe na mitandao ya kijamii wakati wa asubuhi, kwani barua pepe na mitandao hiyo inaweza kukuharibia siku na hivyo kukufanya ushindwe kufanya kazi zako za msingi. Jaribu kufanya mambo hayo kwenye muda wa saa tatu au saa nne hivi ukiwa tayari umeshafanya majukumu yako ya msingi na inakupasa kuangalia mitandao hiyo kwa muda fulani tu kama vile mara tatu kwa siku ili kuwa na muda mzuri wa kutekeleza majukumu yako.

Ingawa tunaishi katika dunia yenye mambo mengi, unatakiwa kujikita katika kazi moja ili kuleta tija na ufanisi wa kazi unayoifanya, kwani kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja kunaweza kukuletea matatizo kama ambavyo wahenga wanasema miluzi mingi humpoteza mbwa.

d) Kazi zako hasa zile ambazo unaona zinakuzidia ama kwa kuwapa wataalamu wakufanyie au kwa kuwapa wafanyakazi walioko chini yako kama unaona wana uwezo wa kufanya hizo kazi.

e) Unatakiwa kusema hapana kwa mambo ambayo hayana tija kwako, kwani si kila fursa inaweza kukufaidisha au kufaidisha biashara yako na kuwa mkweli kwa mambo ambayo unaona yana tija na yasiyo na tija ili kuondoa matatizo yanayoweza kujitokeza baadaye kutokana na mkanganyiko wa taarifa.

f) Thamini muda wako, kwani muda ni kitu cha thamani sana katika maisha au shughuli zako. Jaribu kutenga na kulinda muda wako kwa kufanya vitu ambavyo ni muhimu kwako na kwa biashara yako.

Hata kama utahudhuria kikao ambacho ni muhimu unatakiwa ujue utaanza muda gani na kumaliza muda gani ili uweze kufanya shughuli nyingine muhimu kwani unatakiwa kutumia muda wako mwingi katika kufanya kazi muhimu, zinazohusu shughuli zako/biashara zako.

Kuwa msikivu kwa kila jambo hasa pale unapokuwa unawasiliana na wafanyakazi wako/wenzako au marafiki zako kwani hali hii itakusadia kuelewa mambo yanyohusu shughuli zako na hivyo kuepuka kupoteza muda wa kuomba ufafanuzi wa jambo lilokwisha ongelewa.

Onyesha shukurani kwa kile kilichofanyika kwa mafanikio, huku ukijaribu kukumbuka mafanikio ya kipindi cha nyuma ambayo yatakupa nguvu ya kutenda mambo makubwa zaidi.

Hakikisha kuwa unamaliza kazi zote unazotakiwa kuzifanya katika muda mwafaka ili kesho yake ufanye kazi kwa umakini na kasi inayotakiwa.

Jaribu kusimama na kuzunguka kidogo mahali unapofanyia kazi.

Mwandishi ni mtaalamu wa biashara