Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chadema, Chaumma vinavyopambana kukusanya fedha kwa makada na Watanzania

Muktasari:

  • Chadema kina kampeni ya ‘tonetone’ yenye lengo kukusanya Sh334 milioni zitakazofanikisha kufanyika kwa mkutano wa Baraza Kuu Septemba mwaka huu, wakati Chaumma wanakusanya fedha kupitia operesheni ya ‘tujenge pamoja’ ambazo watazitumia kuendeshea mikutano ya kisiasa kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Dar es Salaam. Vyama vya Chadema na Chaumma, vimeendelea kuchanja mbuga na kampeni za uhamasishaji wananchi kuvichangia fedha kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za uimarishaji wa vyama hivyo.

Chadema kina kampeni ya ‘tonetone’ yenye lengo kukusanya Sh334 milioni zitakazofanikisha kufanyika kwa Baraza Kuu Septemba 2026, wakati Chaumma wanakusanya fedha kupitia operesheni ya ‘tujenge pamoja’ ambazo watazitumia kuendeshea mikutano ya kisiasa kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Hadi leo Jumanne Julai 28, 2026 saa moja asubuhi Chadema kilikuwa kimefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh239.5 milioni zilizochangwa na wanachama wa chama hicho pamoja wananchi mbalimbali.

Wakati Chaumma mkeka wao wa mwisho walioutoa juzi walifanikiwa kukusanya Sh15 milioni tangu kuanza kwa kampeni ya uhamasishaji wananchi na wanachama wa chama hicho kuchanga iliyoanza Julai 21, 2026.

Akizungumza na Mwananchi, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Chadema, Tito Kitalika amewashukuru Watanzania kwa namna wanavyoendelea kujitoa katika kukichangia chama hicho kupitia kampeni ya tonetone.

“Hatuna neno zaidi ya asante kwa Watanzania kwa kile walichokichangia hadi sasa. Kwetu sisi ni kikubwa na kinaandaa mazingira mazuri ya mbele ya chama, tunaamini kama wamechangia fedha hizi ndani ya muda mfupi, basi siku za usoni watatuunga mkono zaidi.”

“Kinacholeta faraja hawa wanaotuchangia wanatoa Sh1,000 au Sh500 ambao ni wengi na watuhakikisha hata tukiingia katika uchaguzi watatuunga mkono,” amesema Kitalika.

Kwa mujibu wa Kitalika, hatua hiyo inaonesha namna ya baadhi ya Watanzania walivyoweka moyo wao kwa Chadema katika kuhakikisha mabadiliko yanapatikana kupitia chama hicho cha upinzani.

“Tuna imani Agosti haitaisha tutakuwa tumefikia kiwango tulichokiweka,” amesema Kitalika.

Chaumma yaendelea kupambana

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi wa Chaumma, Ismail Kangeta amesema mwenendo wa uchangiaji katika chama hicho unakwenda vizuri na wakati wowote wataweka hadharani kiwango kingine kilichopatikana.

Mbali na hilo, Kangeta amesema Chaumma kinaendelea na operesheni ya ‘tujenge pamoja Tanzania ni sisi’ wakianza Tabora, Mpanda na leo Jumanne wapo Jimbo la Kigoma Kusini.

“Tukitoka Kigoma tunakwenda Kagera, Mwanza, Simiyu, Singida, Morogoro, Dodoma kisha Dar es Salaam, kabla ya kwenda Pemba na Unguja,” amesema Kangeta.

Kangeta amesema ziara hiyo, inalenga kuwaunganisha wanachama na Watanzania hasa wakati huu, kuna ajenda ya Katiba Mpya, lakini kabla ya kufika lazima kutambua changamoto zinazowakabili wananchi.

“Tunapozungumza tujenge pamoja, wanaotaka Katiba Mpya, basi wasizuie na wengine wanaotaka bei nzuri kwa wakulima wa pamba,” amesema Kangeta.

Kangeta ameeleza kuwa ziara hiyo, inaongozwa na viongozi waandamizi wa chama hicho, akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Benson Kigaila.