Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kihongosi: Vijana nendeni mkamsemee Rais Samia

Muktasari:

  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Kenani Kihongosi amewataka vijana kumsemea Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Kenani Kihongosi amewataka vijana kumsemea Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo.


Kihongosi amebainisha hayo leo Desemba 23, 2022 wakati wa mapokezi ya mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Ali Mohamed "Kawaida" katika mkoa wa Dar es Salaam.


Amesema Rais Samia ametekeleza miradi mingi ya maendeleo ukiwemo wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ambalo lilianza kujazwa maji jana.


Hata hivyo, amesema vijana hawajitokezi kumsemea Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya, jambo ambalo linawapa nafasi wapinzani kupotosha wananchi.


"Serikali imetekeleza miradi mingi sana, wa kusema ni sisi wanaCCM, vijana twendeni tukaseme.


"Tusikubali wapinzani waende wakapotoshe huko na sisi tupo. Twende tukamtetee Rais wetu, imefika wakati anajitetea mwenyewe, vijana tukamsaidie Rais wetu," amesema Kihongosi.


Wakati huohuo, amesisitiza kwamba uchaguzi katika jumuiya hiyo umekwisha, hivyo amewataka vijana kuungana pamoja kwenda kufanya kazi.


"Uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kuijenga jumuiya na chama chetu, twendeni tukafanye kazi.


"Kwa sasa hakuna timu ya mtu. Mlioshinda mkafanye kazi, ambao kura hazikutosha pia mkafanye kazi, hiki chama hakimtupi mtu anayekitumikia kweli kweli," amesema