Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM Dar kuanza maandalizi ya uchaguzi mwakani

Muktasari:

CCM mkoa wa Dar es Salaam imesema imejipanga kuanza kampeni kwa nguvu mwaka 2023 ili kuhakikisha chama hicho kinashinda nafasi zote katika chaguzi zijazo.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu amesema mwaka 2023 ni wa maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.


Mtemvu ameyasema hayo leo Desemba 23, 2022 wakati wa mapokezi ya mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Mohamed Ali Mohamed ‘Kawaida’ na makamu wake, Rehema Omary katika mkoa wa Dar es Salaam.


Amesema wamejipanga kuanza kampeni kwa nguvu mwaka 2023 ili kuhakikisha chama hicho kinashinda nafasi zote katika chaguzi hizo katika mkoa wake wa Dar es Salaam.


"Tumejipanga, mwaka 2023 ni kampeni asubuhi, mchana na jioni. Mwaka 2024 ni uchaguzi wa serikali za mitaa, ninawahakikishia tutafanya maajabu kwenye uchaguzi ule, tutashinda.


"Mwaka 2025 ni uchavuzi mkuu, tumekubaliana tutachukua madiwani wote wa Dar, wabunge wote Dar na Rais wetu, Samia Suluhu Hassan anapata kura za ushindi," amesema Mtemvu.


Mwenyekiti huyo ambaye alichaguliwa Novemba 2022 akichukua nafasi ya Kate Kamba, amesema atatoa pikipiki tano kwa ajili ya vijana ambapo kila wilaya katika mkoa wake itapata pikipiki moja.


"Kazi kubwa ni hamasa, kuhakikisha vijana wengi wanajiandikisha," amesema Mtemvu huku akishangiliwa na mamia ya vijana waliohudhuria shughuli hiyo ya mapokezi.


Amesisitiza kwamba vijana katika mkoa wa Dar es Salaam wako imara na watawalea na kuwalinda kwa namna yoyote ili wahakikishe wanafikia malengo ya chama