Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana wa kike wahamasishwa kushiriki siasa

Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Rehema Omary

Muktasari:

  • Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Rehema Omary amewahamasisha vijana wa kike kujitokeza kwenye siasa kwa sababu wana uwezo kama vijana wa kiume.

Dar es Salaam. Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Rehema Omary amewahamasisha vijana wa kike kujitokeza kwenye siasa kwa sababu wana uwezo kama vijana wa kiume.


Rehema ametoa wito huo leo Desemba 23, 2022 wakati wa mapokezi ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mohamed Ali Mohamed ‘Kawaida’ katika mkoa wa Dar es Salaam.


Amewataka vijana wa kike kutosubiri kuwezeshwa, bali wajitokeze kwa ujasiri kushiriki katika siasa ikiwa ni pamoja na kuwania nafasi za uongozi.


"Vijana wa kike tujitokeze, tusiogope, tunaweza. Tusisubiri kuwezeshwa, tunaweza kama vijana wa kiume," amesema Rehema.


Amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM kwa kumchagua kuwa makamu mwenyekiti na kuahidi kwamba watakwenda kuwatumikia vijana kwa nguvu zote.


"Tunakwenda kusaka fursa za vijana ili waweze kunufaika kiuchumi, kwa hiyo ni siasa na uchumi. Tuendelee kuchapa kazi na kuishi kwa mshikamano," amesema Rehema huku akishangiliwa na vijana.


Rehema ambaye alikuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Singida, alichaguliwa Novemba 29, 2022 kushika nafasi hiyo baada ya kupata kura 419