Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lukuvi aomba kuchaguliwa amalizie miradi ya maendeleo

William Lukuvi

Muktasari:

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni wa maji, umeme anaotaka ufike katika kila kijiji, kukarabati miundoimbinu ya barabara, vituo vya afya, elimu na kilimo kwa kujenga mabwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Isimani. Aliyekuwa mbunge wa Isimani (CCM), mkoani Iringa, William Lukuvi anayetetea tena kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, amewaomba wakazi wa jimbo hilo kumchagua kwa mara nyingine ili akamilishe miradi ya maendeleo aliyoianzisha.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni wa maji, umeme anaotaka ufike katika kila kijiji, kukarabati miundoimbinu ya barabara, vituo vya afya, elimu na kilimo kwa kujenga mabwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alitoa rai hiyo juzi katika mkutano wa kampeni jimboni humo.

Alisema katika kipindi cha uongozi wake, ametekeleza pia miradi mbalimbali ukiwamo wa maji na kuondoa tatizo sugu lililokuwa linawakabili wapigakura wake.

Lukuvi alisema licha ya maji kuanza kupatikana, bado kuna maeneo ambayo miundombinu yake inapaswa kufumuliwa na kujengwa upya.

Aliwataka wakazi wa Isimani kutofanya makosa katika uchaguzi wa mwaka huu, wawapigie kura wagombea wa udiwani, ubunge na urais kutoka CCM ili waendelee kujengewa miradi mingi zaidi ya maendeleo.

Aliyekuwa mshindani wake kwenye kura za maoni, Hamisa Malinga aliwataka wakazi wa jimbo hilo kumchagua Lukuvi ili atatue changamoto za jimbo hilo.