Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbowe: Polisi msibebe mabomu, yaacheni yaoze huko

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe

Muktasari:

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika mikutano ya chama hicho na kuwataka waendelee kuwajibika katika kulinda raia na mali zao.

  

Songwe. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika mikutano ya chama hicho na kuwataka waendelee kuwajibika katika kulinda raia na mali zao.

Mbowe ambaye leo Jumamosi Februari 25, 2023 amehutubia wananchi wa Mji wa Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe katika Viwanja vya Stendi ya Mwaswala ambapo amesema Jeshi la Polisi japo wanapokea amri, lakini amelishauri kuzipima amri hizo kwani nyingine zinakuwa ni za kuwaumiza wananchi.

"Askari wetu endelea na kazi ya kujenga Taifa kwa kutumia busara, msibebe tena mabomu yaacheni  yaozee huko na yale magari ya washawasha kauzeni huko Kongo, hatutaki gari za washawasha wananchi wanaupole na amani," amesema Mbowe.

Aidha Mbowe amesema suala la mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba hivyo ni vyema haki hiyo ikafuatwa kwani hujenga umoja na kupata changamoto mbalimbali za wananchi.

Awali aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbozi kupitia Chadema, Pascol Haonga amesema vyama vya msingi vya Ushirika vya (AMCOS) vinachangamoto nyingi kwa kuwacheleweshea wakulima hela zao za mauzo ya kahawa.

Haonga amesema  zamani kulikuwa na makampuni kadhaa ambayo yalikuwa yakishindana kwa bei na matokeo yake mkulima ndiye aliyekuwa akinufaika.

"Nilipopeleka hoja bungeni kuhusu zao la kahawa walilikataa na hoja hiyo ilikuwa kuwashauri Serikali kuhusu soko huria katika zao la kahawa kwani miaka ya nyuma tulikuwa na makampuni yanayonunua kahawa hapa Mbozi ,makampuni kama Domani, Lima kitu ambacho kilikuwa kinampa mkulima faida.

"Kampuni hayo yalikuwa yakishindana kwa bei ya kununua kahawa, lakini kwa sasa kuna changamoto nyingi katika hizi Amcos. Kuna baadhi ya Amcos zimekusanya kahawa tangu mwaka jana mwezi wa saba na hadi sasa wakulima hawajalipwa fedha zao," amesema.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Kanda ya Mara, John Heche amesema kama wananchi watawaparidhaa kuongoza watavunja mfumo wa Serikali wa kuwa na viongozi wengi wa kiserikali na kuleta mfumo wa Serikali za majimbo ambapo kutakuwa na Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na mawaziri wachache wa kitaifa.

Amesema kila jimbo litakuwa na kiongozi wake kama Waziri wa Kilimo kuwepo kwenye kila Jimbo na sio waziri mmoja anahudumia nchi nzima.