Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msigwa kuungana na Lema, Sugu, Boni Yai jukwaani Morogoro

Muktasari:

  • Ujio wa viongozi wa kitaifa wa Chadema wakiongozwa na Godbless Lema na Salma Kasanzu unatajwa kufungua ukurasa mpya wa uhai wa chama hicho mkoani Morogoro.

Morogoro. Mchungaji Peter Msigwa, aliyerejea Chadema, anatarajiwa kuhutubia katika mikutano ya hadhara mkoani Morogoro akiwa pamoja na Godbless Lema, Joseph Mbilinyi (Sugu) na Boniface Jacob, maarufu Bon Yai, katika operesheni ya ‘Free Tundu Lissu na Katiba Mpya’.

Ujio wa viongozi hao unatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa Chadema kuimarisha uhai wake wa kisiasa mkoani humo.

Juni 30, 2024 Msigwa alitangaza kujiunga CCM mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ikulu jijini Dar es Salaam na katika uchaguzi mkuu 2025 alikuwa miongoni mwa makada waliokuwa wanasaka ushindi wa CCM.

Hata hivyo, Mei 23,2026 Msigwa alitangaza kurejea Chadema kwa kile alichodaiwa ametafakari kwa kina kisha kufikia uamuzi huo.

Akizungumza na Mwananchi leo Juni 10, 2026, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Jackson Malisa, amesema kabla ya kuanza kwa mikutano ya hadhara kutafanyika kikao cha ndani cha baraza la mashauriano kitakachowakutanisha wajumbe kutoka majimbo yote 11 ya mkoa huo na wilaya zake 14.

Malisa amesema kikao hicho kitasaidia kufanya tathmini ya hali ya chama na kuweka mikakati mipya ya kuimarisha shughuli za kisiasa katika mkoa huo.

Amesema ratiba ya operesheni hiyo inaonesha kuwa mikutano itaanza Juni 16 katika Jimbo la Kilombero kwenye Uwanja wa Mwembe Chadema Ifakara, Juni 17 Kata ya Ruaha katika Jimbo la Mikumi, Juni 18 mkutano mkubwa katika Manispaa ya Morogoro na Juni 19 kuhitimishwa katika Jimbo la Gairo.

Mbali na Msigwa, Lema, Sugu na  Jacob, viongozi wengine wanaotarajiwa kushiriki katika ziara hiyo ni Salma Kasanzu, Deogratias Mahinyila na Ashura Masoud.

Kwa upande wake, Katibu wa Wazee wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Monica Mushi, amesema ujio wa viongozi hao utachochea hamasa mpya kwa wanachama wa chama hicho.