Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Othman Masoud ataka mambo aliyopigania Maalim Seif yafanyiwe kazi

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman

Muktasari:

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amesema ipo haja ya kutafakari na kufanya tathmini ya kuangalia mambo aliyoyapigania Maalimu Seif Sharif Hamad kama yanafanyiwa kazi ili kupata mwelekeo wa pamoja.

  

Unguja. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amesema ipo haja ya kutafakari na kufanya tathmini ya kuangalia mambo aliyoyapigania Maalimu Seif Sharif Hamad kama yanafanyiwa kazi ili kupata mwelekeo wa pamoja.

Miongoni mwa mambo aliyoyapigania Maalim Seif ambaye alikuwa mwenyekiti wa ACT- Wazalendo enzi za uhai wake ni usawa, haki sawa, utawala bora, uchumi imara na siasa safi.

Hata hivyo, Othman amesema hivi sasa watu wanaona mambo yanakwenda vizuri lakini ukiangalia kwa undani mifumo hasa ya elimu, afya na mengineyo bado haipo katika mazingira ya kumuandaa kijana aweze kukabiliana na changamoto za sasa na baadaye.

Ameelea hayo leo Jumamosi Oktoba 22, 2022 wakati akifungua mkutano wa pili wa Taasisi ya Maalim Seif unaolenga kumuenzi kiongozi huyo aliyefariki dunia Februari 17, mwaka jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Katika mkutano huo, Masoud alikuwa anazungumzia elimu bora katika kujenga watoto werevu, nini kimekosekana Zanzibar na namna ya kurekebisha.

“Tunaposema tuwe na amani, kuwe na utulivu na maridhiano ni kwa sababu hayo ndio yatakayojenga uchumi imara utakaoweza kukabiliana na changamoto kama hizi.

“Tunapozungumza kuna changamoto za Muungano zitatuliwe ili Zanzibar iweze kusimama kiuchumi ni kwa sababu mambo kama haya yanayotakiwa kuangaliwa kwa undani.

“Kwa sasa tumejiachia na kuona kila kitu kinakwenda vizuri lakini tukifanya tathmini na tafakuri bila shaka tutagundua kuna changamoto,” amesema Othman.

Amesema iwapo mambo hayo yakifanyiwa uchunguzi wa kina watu watajua kwa nini Maalim Seif alijitoa  muda wote kuipigania Zanzibar yenye amani, utulivu, maridhiano, uchumi na utawala bora.

Othman amesema kuna kazi kama viongozi kuweza kukabiliana changamoto hizo ili kusaidia vizazi vya sasa na vijavyo