Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wataja mapendekezo Bunge maalumu

Jphn Mnyika

Muktasari:

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika alisema wajumbe wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya siyo na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), kimepitia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mbalimbali huku kikitoa mapendekezo yake kupinga Rais kuteua Wajumbe wa Bunge Maalumu wasiotokana na Bunge au Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika alisema wajumbe wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya siyo na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi.

“Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi zao kuwawakilisha katika Bunge la Katiba kwa sababu Muswada Mpya unapendekeza wateuliwe na Rais.”

Kwa sababu ya upinzani huo, mapendekezo ya kumfanya Rais kuwa mteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu wasiokuwa wabunge na Wawakilishi yaondolewe katika Muswada huo wa Sheria. Badala yake, kifungu cha 22(1)(c) cha Sheria iliyotungwa na Bunge kiliweka wazi kwamba “wajumbe 166 [watateuliwa] kutoka ...” taasisi zilizotajwa katika kifungu hicho.

Mnyika alisema kuwa Chadema inapendekeza kwamba “Sheria iweke wazi kwamba wajumbe hawa ‘watateuliwa na’ taasisi zilizotajwa. Hii itaondoa utata juu ya uwakilishi wao na juu ya mamlaka yao ya uteuzi.”

Akizungumzia Wabunge au Wawakilishi wa Zanzibar alisema: “Hii ni kwa sababu aya ya 3 ya Muswada inapendekeza kwamba wajumbe hao sasa wateuliwe na Rais. Hiyo ni sawa na kusema kwamba kilichokuwa hakifai miaka miwili iliyopita sasa kinafaa na kilichokataliwa wakati ule sasa kinakubalika!

“Ili kuficha ukweli kwamba mwenye mamlaka ya uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu wasiokuwa Wabunge au Wawakilishi ni Rais, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Muswada unapendekeza kuongezwa kwa vifungu vidogo vipya viwili katika kifungu cha 22.

“Kwanza, inapendekezwa kuwe na kifungu kidogo cha (2A) ambacho kitamruhusu Rais kualika kila kundi lililoainishwa katika kifungu kidogo cha 1(c) “kuwasilisha kwake orodha ya majina ya watu wasiozidi watatu.”

‘‘.

ili kuteuliwa kuwa wajumbe.” Pili, inapendekezwa kuwe na kifungu kidogo cha (2B) kitakachomlazimu Rais kuzingatia sifa na uzoefu wa watu waliopendekezwa, na usawa wa jinsia wakati wa kufanya uteuzi wa wajumbe hao.