Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benki zina majukumu mengi zaidi ya mikopo

Siyo jambo la kushangaza kusikia karne hii ya 21 ya sayansi na teknolojia mtu hajawahi kukanyaga mlango wa benki yoyote iwe ya biashara, kilimo au uwekezaji.

Nilipata nafasi ya kufanya kazi na benki kadhaa za biashara hapa nchini, na nilipokuwa katika kutimiza majukumu yangu nilikutana na watu walionieleza kwamba hawajawahi kuingia benki. Siyo kwa sababu wanapaogopa, ila hawana taarifa nini cha ziada benki inafanya mbali na kutunza pesa na kutoa mikopo.

Maendeleo ya mtu na Taifa kwa ujumla yanategemea ushirikishwaji wa jamii katika mfumo wa taasisi za kifedha.

Taasisi za kifedha zipo kwa ajili ya kutatua changamoto za kifedha kwa watu, hivyo ni muhimu jamii ikashirikiana kujenga uchumi imara kwa Taifa na jamii kwa jumla.

Hapa nitakueleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki kisheria japo wengi wanafahamu mbili tu, yaani kutunza fedha na kutoa mikopo.

Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya 2006 kifungu cha 24(1), imetaja shughuli hizo kwa benki yenye leseni ya biashara.

Kupokea amana; hii ndiyo kazi kubwa na ya kwanza kwa benki na ndiyo msingi wa mambo mengine yote.

Benki haitaweza kujiendesha kama haina amana za kutosha kwa sababu amana huongezeka kunapokuwa na ongezeko la akaunti mpya au uwekaji mzuri wa akiba kwa wateja.

Kukopesha; ni moja wapo ya majukumu ya msingi ya benki,ni namna ambayo amana iliyowekwa na wateja wenye akiba au ziada inapewa kwa wateja wenye uhitaji (mikopo) kwa gharama fulani(riba). Mikopo inaweza kuwa binafsi, biashara au kilimo pia unaweza kuwa wa muda mfupi au muda mrefu.

Huduma za kutuma na kupokea fedha; hii ni moja ya jukumu la benki. Katika huduma hii benki inampa fursa mteja au ambaye si mteja kutuma fedha ndani na nje ya nchi.

Kupitia huduma hii rafiki mteja hana haja ya kuwa na akaunti kila benki kufanya malipo anaweza kumlipa mtu asiyekuwa wa benki yake yaani mfano mnunuzi aliyefungua akaunti benki moja anaweza mlipa muuzaji aliye benki nyingine.

Kutoa na kusimamia za malipo; mzunguko wa fedha unakwenda sambamba na mauzo na ununuzi hali inayosababisha uhitaji wa malipo kufanyika kwa usalama. Taasisi za fedha zinampa fursa hiyo, mteja wa benki ambaye ni mtu wa kawaida.

Taasisi au kampuni inaweza kuiomba benki kufanya malipo badala ya kwenda kwa wateja wake, kwa mfano kampuni inaweza kuwalipa wafanyakazi wake kupitia benki kwa kuwaandikia hundi wakalipwa au kuwafungulia akaunti halafu benki itatoa hela moja kwa moja kwenye akaunti ya mwajiri kwenda kwa waajiriwa kwa kufuata ombi la mwajiri.

Huduma ni salama na imeleta mapinduzi makubwa hivyo kusababisha mzunguko wa fedha kwenda kwa kasi nzuri inayoridhisha.

Dhamana na usimamizi; benki pia inaweza kusimama kama dhamana kwa mteja wake anayetaka kufanya ununuzi pasipo kulipa papo hapo.

Kwa mfano, mteja wa benki fulani anataka kununua bidhaa kutoka nje ya nchi lakini hawezi kulipa papo hapo anaweza kuitembelea benki ya biashara akaiomba isimamie kama dhamana yake kwenye ununuzi huo.

Kama atakidhi vigezo, basi benki itawasiliana na benki ya muuzaji nje ya nchi ili bidhaa zitumwe kwa mnunuzi. Kwa kufanya hivyo benki itakuwa imemdhamini mteja wake na kusimamia ununuzi wa bidhaa.

Kubadili fedha za kigeni; hili siyo jambo la kushangaza kumuona mtu anazunguka mijini akitafuta sehemu ya kubadili fedha za kigeni na akizipita benki.

Fahamu kuwa benki zipo kwa kazi hiyo, unapokuwa na fedha ambazo siyo za Kitanzania ni vyema ukatembelea benki yoyote iliyokaribu nawe kupata huduma hiyo japokuwa pia ni vizuri kuzingatia vigezo na masharti.

Ushauri wa fedha na biashara; mteja wa benki siyo lazima awe ana akaunti na benki ili apewe ushauri, kwa kuwa unaweza kuwa ni wakiukezaji katika masoko ya fedha.

Utunzaji wa vitu vya thamani; kinachoifadhiwa benki siyo fedha tu, bali hata vitu vingine vinavyohitaji usalama kama vito, madini, vyeti, wosia, hati za nyumba na magari na nakala au mikataba huku vikilipiwa gharama inayokubalika kisheria.

Huduma hii ni nzuri hasa ukuzingatia mahala tunapoishi kwenye miji yetu hakuna usalama wa kutosha kukaa na vitu vyenye thamani kubwa vinavyoamsha hisia za matamanio ya wizi.

Ubadilishaji fedha; ikumbukwe kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hutumia benki za biashara kurekebisha mzunguko wa sarafu na noti nchini.

Hivyo kupitia benki za biashara mteja anaweza kwenda benki na noti na kuomba kupewa sarafu zenye thamani sawa bila makato yoyote lakini benki kuu uzikusanya noti chakavu kupitia benki za biashara nakurudisha noti mpya kupitia mfumo huu.

Uchambuzi huu umeandikwa na mkufunzi wa Chuo Kikuu Ardhi anayepatikana kwa namba +255 765 666 255