Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi inarejea kila mmoja atimize wajibu wake

Jumatano iliyopita, dirisha dogo la usajili hapa Tanzania kwa msimu huu lilifungwa rasmi baada ya kutimia kwa mwezi mmoja tangu lilipofunguliwa Desemba 16 mwaka jana.

Idadi kubwa ya timu hazikufanya usajil wa wachezaji wengi na hiyo inaonyesha kuwa wachezaji ambao ziliwasajili kabla ya kuanza kwa msimu wengi wamefanya vizuri hivyo mabenchi yao ya ufundi hayakuona haja ya kunasa wachezaji wengi.

Wakati dirisha dogo la usajili likifungwa, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilitangaza kurejea kwa Ligi Kuu Bara ambayo iliahirishwa kupisha fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (Chan) 2024 ambazo awali zilipangwa kuchezwa kuanzia Februari Mosi hadi Februari 28 mwaka huu.

Matamanio ya kila mmoja sasa ni kuona wachezaji waliosajiliwa wanakwenda kuziwakilisha vyema klabu zao katika ligi ili iweze kuwa na ushindani na  mvuto wa hali ya juu.

Ili hilo litokee, makundi manne muhimu kila moja kutimiza wajibu wake ili wachezaji waweza kufanya vizuri na mwisho wa siku kuchangia mafanikio ya timu katika mashindano tofauti.

Makundi hayo manne ni wachezaji  wenyewe, makocha kwa maana ya mabenchi ya ufundi, viongozi na mashabiki.

Haya yanapaswa kuzungumza lugha moja ili mambo yaende vizuri na kama yakishindwa basi hakutakuwa na uwezekano wa klabu kuwa na utulivu na pia kuleta faida chanya kama inavyokusudiwa.

Wachezaji wanatakiwa kuwajibika kwa kuhakikisha wanafanya mazoezi ya kutosha, kujiweka kando na mitindo mibaya ya maisha ambayo inaweza kuathiri vipaji na ufanisi wao mazoezini jambo ambalo huwa chanzo cha timu kufanya vibaya na kushindwa kutimiza malengo ambayo imejiwekea.

Mfano wa mitindo mibaya ya maisha ambayo wachezaji wanatakiwa kuikwepa ni ngono zembe, ulaji wa wa vyakula usiozingatia program za lisha lakini pia matumizi ya dawa za kulevya na zile za kuongeza nguvu.

Ulaji usiozingatia program za lishe unaweza kupelekea kuongezeka kwa uzito wa mchezaji na hivyo kumfanya ashindwe kutoa mchango mkubwa kwa timu kama ilivyo kwa matumizi ya dawa za kulevya.

Kundi la pili ambalo linapaswa kuwajibika ni maofisa wa benchi la ufundi ambalo linakuwa chini ya usimamizi wa kocha na wasaidizi wake.

Hawa ndio watoa ramani wa nini timu inatakiwa ikifanye na katika namna gani ili iweze kutimiza kile ilichopanga kukifanya kuendana na ubora na udhaifu wa wapinzani ambao inakutana nao.

Makocha wana nafasi kubwa ya kulinda ubora wa wachezaji, kuwapandisha au kuwashusha viwango vyao kutegemeana na ubora wa program na mbinu wanazowapa au namna ambavyo wanatumia ufundi wao hivyo kama wakiifanya vyema kazi yao, tutegemee kuna ushindani wa hali ya juu katika mechi zilizobakia za ligi.

Tunatamani kuona makocha wakitupa mechi nzuri pindi ligi ikirejea huku timu na wachezaji wakionyesha kile ambacho wamekifanyia kazi katika viwanja vya mazoezi.

Muunganiko mzuri wa makocha na wachezaji ili upatikane ni lazima upande wa uongozi ukafanya yale ya msingi ya kiutawala kwa wakati sahihi na njia za kiweledi.

Uongozi unapaswa kuhakikisha timu inapata huduma stahiki kama vile malazi, matibabu, mishahara na posho na pia usafiri kutoka kituo kimoja cha mchezo kwenda kingine.

Wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi wanahitaji kuwa katika mazingira tulivu ambayo yatawafanya wafanye kazi yao vizuri na  hilo litawezekana ikiwa viongozi watawapatia huduma wanazohitaji mapema na sio kwa kuwacheleweshea.

Ni ngumu kwa mchezaji kujitoa kwa asilimia 100 uwanjani ikiwa hajapata mshahara na posho zake kwa wakati na mara nyingi husababisha migogoro ya mara kwa mara baina ya viongozi na wachezaji ambayo hudhoofisha zaidi timu badala ya kuiimarisha.

Kundi lingine ambalo nalo lina wajibu wa kufanya mechi zilizobakia za ligi kuwa zenye mvuto, ushindani na msisimko ni mashabiki.

Shabiki ni mchezaji wa 12 ndani ya uwanja. Uwepo wake uwanjani unamhasisha mchezaji kujitoa na kucheza kwa ari kwa ajili ya timu.

Timu inaweza kuwa na wachezaji wazuri, benchi bora la ufundi na uongozi mzuri lakini kama inakosa mashabiki, inaweza isifanye vizuri kwa vile wachezaji wanakosa watu wa kuwajibika kwa ajili yao.

Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia namba ndogo ya mashabiki ambao wamekuwa wakijitokeza kutazama mechi za Ligi viwanjani jambo ambalo limekuwa likizinyima timu hamasa ya kutosha lakini pia mapato ambayo huwa yanatokana na viingilio vinavyolipwa na mashabiki hao kwenda uwanjani.

Kwa nchi ambayo kwa sasa inaheshimika na kutazamwa kuwa ya kisoka kama Tanzania, mashabiki wanapaswa kuanza kurudi kwa winhi viwanjani pindi ligi itakaporejea mwanzoni mwa Februari.

Watu waende kuzisapoti klabu zao kwa kuzishangilia kuzipa hamasa wakati huohuo wakiziwezesha kifedha kupitia viingilio vya milangoni.

Pia shabiki anapokuwepo uwanjani anaongeza hamasa kwa wachezaji na kuwafanya wajione wana deni na wanatakiwa kucheza kwa bidii ili kuiwezesha timu kufanya vizuri.

Ligi yetu kwa sasa iko katik nafasi ya sita katika chati ya ubora barani Afrika hivyo kuna uwezekano ikapiga hatua zaidi iwapo makundi hayo manne tajwa hapo juu yataungana kwa pamoja na kila moja likafanya vyema kile ambacho linatakiwa kutimiza.