Tanesco ukataji huu wa miti mitaani mnatukosea

Sunday May 02 2021
Tanesco pc

Mhariri,

Hongera kwa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kwa kazi nzuri mnayofanya.

Ingawa bado mnatakiwa kuongeza juhudi, kwani katika baadhi ya maeneo upatikanaji wa umeme ni changamoto ya kudumu, huku wengine wakilalamika kukatikakatika kila mara.

Mbali na hayo, mnafanya kazi nzuri. Nimejitokeza kuandika barua hii leo kulalamikia mnachokifanya mitaani. Mnapokata miti bila kuwahusisha wamiliki wake bila kujali ni ya matunda au kivuli.

Kuna ambayo kweli ipo mahali ambako inahatarisha usalama wa miundombinu ya umeme, lakini kwingine mnakata tu kwa sababu mna msumeno.

Hii si sawa, hususan mnapokata miti ya matunda ambayo wahusika wametumia nguvu nyingi kuiotesha.

Advertisement

Gabriel Ngaiza, DSM

Advertisement