Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF fanyieni kazi changamoto za Lligi Kuu Bara

Muktasari:

Huu ni wakati ambao viongozi wanaumiza kichwa kuandaa timu na kuweka sawa baadhi ya kasoro ambazyo yalijitokeza  msimu uliopita.

Maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi yanaendelea kupamba moto na timu mbalimbali zinaendelea kujiimarisha kuwa na vikosi bora ambavyo himili ushindani.

Huu ni wakati ambao viongozi wanaumiza kichwa kuandaa timu na kuweka sawa baadhi ya kasoro ambazyo yalijitokeza msimu uliopita.

Wapo ambao licha ya kupambana usiku na mchana ili kuangalia wachezaji ambao wanaweza kuongeza nguvu kwenye timu zao, wapo viongozi na timu nyingine ambao wazimekuwa kwenye harakati ya kutafuta wadhamini ambao watawazisaidia kujiongezea nguvu ya kiuchumi ambayo itawafanya waweze kumudu gharama za kujiendesha kwenye ligi.

Pamoja na juhudi hizo kubwa zinazofanywa na klabu mbalimbali, bado nadhani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linatakiwa kukitumia kipindi hiki kufanyia kazi masuala na changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye msimu uliopita ili zisiweze kujirudiea kwenye msimu ujao.

Miongoni mwa changamoto hizo ni suala la upangaji mbovu wa ratiba za mechi kwa timu za Ligi Kuu na zile za Ligi Daraja la Kwanza.

Ni lazima ratiba kwa ajili ya msimu ujao iwe ni ile ambayo itaziwezesha timu kufika kwenye vituo vya mchezo kwa wakati bilapasipo kuathiri ratiba ya michezo inayofuata ya timu husika au nyingine.

Tulishuhudia msimu uliopita ratiba ya ligi ikibadilishwa ghafla mara kwa mara na kuziathiri timu kiuchumi hata kiufundi. Mabadiliko hayo ya ratiba wakati mwingine hayakuwa ya msingi na jambo lililosababishapelekea watendaji wa juu wa TFF sambamba na wale wa Bodi ya Ligi Kuu kushindwa kutoa sababu makini za kutetea kwa nini yalifanyika.

Timu kama Tanzania Prisons kwa mfano, ilitoka mkoani Mbeya kuja jijini kucheza na Azam FC kwenye mchezo ambao tayari ulishakuwa kwenye ratiba ya ligi. Cha ajabu siku mbili kabla ya pambano hilo, Prisons iliamrishwa kurejea jijini Mbeya kucheza na Yanga kwenye mchezo wa kiporo halafu irejee tena jijini kucheza na Azam.

Jambo kama hilo si zuri kwenye mchezo wa soka kwani ilikuwa ni kuiumiza Prisons ambayo ililazimika kusafiri umbali wa zaidi ya kilomieta 2,000 kucheza mechi hizo mbili ndani ya kipindi cha siku zisizozidi tano.

Ukiondoa changamoto ya ratiba, suala jlingine ambalo liliitia doa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita ni uamuzi mbovu wa baadhi ya waamuzi ambao walipewata dhamana ya kusimamia nafasi ya kushika kipyenga kwenye mechi za ligi hizo.

Ingawa TFF kupitia kamati yake ya waamuzi inayoongozwa na Mwenyekiti Salum Chama imekuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha waamuzi wanachezesha kwa kuzingatia kanuni 17 za mchezo wa soka, bado kuna baadhi  ambao waliokuwa kero kubwa katika ligi hizo.

Waamuzi hao ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya, walipindisha sheria za soka hali iliyosababishapelekea kupatikana kwa matokeo yaliyoziumiza timu ambazo kwa hakika zilistahili kupata matokeo mazuri kutokana na maandalizi mazuri ambayo zilifanya kwa ajili ya ligi.

Wapo baadhi yao ambao walikuwa wakichezesha kwa mapenziau ushabiki kwa timu fulani, hivyoali kuiliyoashiria kama vile walikuwa tayari na matokeo yao mifukoni.

Upuuzi na ujinga huo wa baadhi ya waamuzi kwenye mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza, ndiyo ambao kwa asilimia kubwa ulichangia vurugu katika baadhi ya mechi, ambazo zilisababisha waamuzi wapate vipigo vilivyohatarisha maisha yao pamoja na mashabiki waliojitokeza viwanjani.

Kero nyingine ni ile ya uduni wa viwanja ambavyo vilikuwa vinatumika kwa michezo ya ligi. Usalama kwenye viwanja vingi ulikuwa mdogo na havikuwa na hali nzuri ya kuwawezesha  na wachezaji kuonyesha viwango vyao.

TFF inatakiwa kukitumia vyema kipindi hiki, kukutana na wadau wa ligi ambao ni timu, wadhamini na mashabiki ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kuondoa changamoto hizo ambazo zilijitokeza kwenye ligi msimu uliopita.

Kama ilivyo kwa viongozi wa klabu mbalimbali ambao sasa wanahangaika usiku na mchana kurekebisha hali ya mambo ndani ya timu zao, watendaji wa TFF sambamba na wale wa Bodi ya Ligi hawapaswi kulala kwenye kipindi hiki, bali wanatakiwa wakitumie kikamilifu kuona wanawezaje kuondoa changamoto hizo zilizofanya msisimko wa ligi msimu uliopita kupungua.

Tunajua TFF imejitahidi kwa asilimia kubwa kuhakikisha ligi yzetu zinaendeshwa kwa mfumo bora na wa kisasa, lakini bado kuna mambo fulani ambayo bado yanahitaji juhudi za dhati kutoka kwa shirikisho.

Haitokuwa jambo jema kuona watendaji wa TFF wanakitumia kipindi hiki cha maandalizi kuelekea msimu ujao wa ligi  hakuna kukaa pale Karume na kupiga soga, badala ya kwenda mikoani na kukagua matunzo ya viwanja mbalimbali ambavyo vitatumika na timu kwa michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza.

Hiki ni kipindi kifupi  ambacho kama kikitumiwa vizuri na watendaji hao, msimu ujao utakuwa bora zaidi ila kama hakitaotumika ipasavyo kumaliza changamoto zilizojitokeza msimu uliopita, basi tutakuwa na ligi mbovu ambayzo hazitokuwa na faida kwa maendeleo ya soka letu.