Alichoandika Morrison baada ya kuishinda Yanga CAS

Bernard Morrison

Muktasari:

  •  Jana Jumatatu ilitolewa hukumu ya kesi iliyokuwa inamhusu mchezaji wa Simba, Bernard Morrison iliyofunguliwa na waajiri wake wa zamani, klabu ya Yanga. Huku hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa soka juu ya sakata lililohusu usajili wa mchezaji huyo kwenda Simba huku Yanga wakidai bado ni mchezaji wao, ilitolewa na kupokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki na wadau wa soka.


Dar es Salaam. Jana Jumatatu ilitolewa hukumu ya kesi iliyokuwa inamhusu mchezaji wa Simba, Bernard Morrison iliyofunguliwa na waajiri wake wa zamani, klabu ya Yanga. Huku hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa soka juu ya sakata lililohusu usajili wa mchezaji huyo kwenda Simba huku Yanga wakidai bado ni mchezaji wao, ilitolewa na kupokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki na wadau wa soka.

Hata hivyo baada ya hukumu  hiyo, iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Michezo (Cas) iliyoitaka Yanga kumlipa kiungo wa Simba, Bernard Morrison Sh12 milioni, Yanga waliipokea na kukubaliana na matokeo.

Kwa upande wa mchezaji huyo, baada ya hukumu hiyo aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram akiishukuru Yanga ambao ndio walimleta Tanzania chini ya Kocha Luc Aymael na ujumbe wake huo ulisomeka;

"Kuna mwanzo na mwisho wa kila kitu, hakuna kinachodumu milele, Tumekuwa tukisubiri hukumu (iwe nzuri au mbaya) mwisho umefika na kumaliza dukuduku.
Nataka kila mmoja ajue jinsi nawashukuru Yanga kwa kunipa nafasi na kuvaa jezi yao, hakuna mtu hapa Tanzania aliyenijua wala kujali kuhusu kipaji changu hadi kocha Luc Aymael aliponileta nicheze. Asante sana kocha kwa kuniamini na kunifanya mchezaji mkubwa.

Kuna msemo Ghana unasema ' Dokta mbaya anayekupa huduma hadi dokta mzuri akafika anahitaji kupongezwa' hata kama alikuwa mbaya alikufanya uwe hai hadi yule mzuri alipofika. Kwa hiyo rasmi niseme nawashukuru Yanga na yeyote aliyenifanya nitabasamu na kunipenda nikiwa Yanga, bila kusahau upendo wa mashabiki."Morrison