Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshahara kukwamisha dili la Maguire

Manchester, England. Mabosi wa Manchester United wapo kwenye wasiwasi mkubwa ikiwa wataweza kumuuza beki na nahodha wao, Harry Maguire kutokana na mshahara wake.

Taarifa kutoka mtandao wa Football Insider umethibitisha kwamba hivi karibuni kocha Erik ten Hag alikutana na bodi ya timu hiyo na kuiambia nyota huyo auzwe kwenye dirisha lijalo.

Kuuzwa kwa Maguire ni moja kati ya mipango ya Mashetani Wekundu katika kuhakikisha kwamba wanaimarisha zaidi kikosi chao tofauti na msimu huu.

Changamoto kubwa ni kwamba ili Maguire ajiunge na timu nyingine kwenye dirisha lijalo, ni lazima timu husika ikubali kumpa mshahara wake wa Pauni 200,000 kwa wiki anaopokea kwa sasa akiwa na Man United.

Kiasi hicho cha fedha ndiyo kinaonekana kuwa changamoto kutokana na kiwango cha beki huyo wa kimataifa wa England kwa sasa.

Mkataba wa Maguire aliyejiunga na Man United mwanzoni mwa msimu wa 2019/20 kwa Pauni 80 milioni, mkataba utakaomalizika 2025.

Kwa sasa Paris Saint-Germain ndiyo inatajwa kuwa kwenye uhitaji mkubwa zaidi na huduma yake ili akawe mbadala wa Sergio Ramos, ambaye huenda akaondoka mwisho wa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika.

Hata hivyo, PSG kwa sasa inapambana kubana matumizi ili kuepuka rungu la sheria za matumizi ya fedha kutoka FIFA, hivyo inahitaji kulipa mishahara ambayo haitokuwa mikubwa sana na ina mpango wa kumlipa beki ajaye mshahara ambao hautozidi ule wa sasa wa Ramos ambao ni Pauni 225,000.

Hadi sasa, Maguire amecheza jumla ya mechi 21 za mashindano yote na kati ya hizo ni mechi 10 tu ndizo alianza kwenye kikosi cha kwanza.

Timu kadhaa kutoka England pia zimetajwa kutaka kumsajili nyota huyu ikiwa pamoja na West Ham, lakini changamoto kubwa inaonekana kuwa katika mshahara wake.