Angetile atajwa mkandarasi wa soka wa Kichina

Muktasari:
"Uwepo wa watu kama hawa kwenye mkutano mkuu wa TFF ni heshima kubwa na wanapaswa kupewa thamani kutokana na kazi walioifanya, naheshimu kukuona hapa Angetile na kukubali mwaliko huu,"
KATIBU wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah ametajwa kama mkandarasi wa soka wa Kichina kutokana na kazi aliyoifanya kwenye uongozi wake.
Naibu Waziri wa mambo ya nje ya nchi,Damas Ndumbaro amesema kati ya viongozi anaowakumbuka katika uongozi wa TFF, Angetile ni mmoja wao.
"Uwepo wa watu kama hawa kwenye mkutano mkuu wa TFF ni heshima kubwa na wanapaswa kupewa thamani kutokana na kazi walioifanya, naheshimu kukuona hapa Angetile na kukubali mwaliko huu,"
"Nakuona Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla nitakwambia kwa nini Angetile nimemuita Mkandarasi wa soka wa Kichina baada ya kumaliza mkutano huu na tukiwa wawili," amesema.