Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal tayari ina majina mezani

Muktasari:

  • Kuumia kwa Kai Havertz na Bukayo Saka pia kulizidisha matatizo, huku Mikel Merino akilazimika kucheza kama mshambuliaji wa kati kwa muda ili kuziba pengo.

London. Mchakato wa  Arsenal kumsajili mshambuliaji mpya wa pembeni na kuboresha safu yao ya ushambuliaji unaendelea ambapo kocha Mikel Arteta na mkurugenzi wa michezo Andrea Berta wanadaiwa kuwa na majina kadhaa tayari.

Arsenal  ilikosa taji la Ligi Kuu England msimu uliopita,kwa tofauti ya pointi 10 nyuma ya mabingwa Liverpool, na kushindwa kufikia kiwango chao cha msimu wa 2023-24 na moja ya sababu zilizochangia ilikuwa ni  kiwango kibovu kilichoonyeshwa na safu yao ya ushambuliaji.

Kikosi cha Arteta kilifunga mabao 22 pungufu katika mechi 38 msimu huu ikilinganishwa na mwaka jana ingawa pia ilipoteza idadi sawa ya mechi kama Liverpool ya Arne Slot, na kutoa sare 14.

Kuumia kwa Kai Havertz na Bukayo Saka pia kulizidisha matatizo, huku Mikel Merino akilazimika kucheza kama mshambuliaji wa kati kwa muda ili kuziba pengo.

Hiyo imesababisha Arsenal kupambana sana kuhakikisha inaimarisha safu ya ushambuliaji katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

 Eneo la kwanza ambalo Arsenal inataka kuliboresha ni mshambuliaji mpya wa kati (namba tisa) ambapo wanahitaji huduma ya Benjamin Sesko wa RB Leipzig na Viktor Gyokeres wa Sporting Lisbon wanaonekana kuwa watampa ushindani Havertz katika nafasi ya mshambuliaji.

Sesko amekuwa chaguo la kwanza kwa sasa, lakini Gyokeres bado yupo kwenye mipango yao licha ya kuwa dili lake limeingia katika sintofahamu baada ya staa mwenyewe kupishana na viongozi wa Lisbon.

Arsenal pia inaendelea na harakati za kusajili winga bora wa kushoto, upande wa kulia tayari wana  Saka na upande wa kushoto kuna  Gabriel Martinelli lakini anaonekana amepungua makali baada ya kufunga mabao machache katika misimu miwili iliyopita ikilinganishwa na msimu wa 2022-23.

Arteta anaamini huu ndio wakati wa kumsajili mchezaji mwingine wa nafasi yake  mwenye kiwango cha juu anayeweza kumpa ushindani.

Winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, naye alikuwa katika rada za Arsenal lakini sasa anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kujiunga na Barcelona ingawa dili bado halijakamilika.

Eberechi Eze pia yupo kwenye rada za Arsenal, lakini wanajua anapendelea kucheza katikati zaidi badala ya winga, pia ili kumwachia Crystal Palace inataka ada ya pauni 68 milioni ilipwe kwa pamoja jambo linaloonekana kuwa gumu kwa Arsenal.

Lakini timu hiyo ya Kaskazini mwa London pia imekuwa ikimfuatilia kwa karibu winga wa Real Madrid, Rodrygo na ina matumaini kuwa wanaweza kufanikisha dili hilo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil anagharimu takriban pauni 70 milioni na hivi karibuni anaripotiwa kuomba kuondoka kwa sababu haoni kama atapata nafasi chini ya kocha mpya Xabi Alonso pale msimu utakapoanza.