Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta ampa Saka ufalme wa Messi

Muktasari:

  • Arsenal iliibuka na ushini wa mabao 2-0 katika mchezo huo ambao Saka alipika bao moja na kufunga bao moja la ushindi baada ya lile la Kai Hevertz.

LONDON, ENGLAND. Juzi Jumamosi Arsenal ilikuwa uwanjani dhidi ya Wolves mchezo wa kwanza kwa timu hizo wa Ligi Kuu England, lakini kile alichokiona Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta kwa nyota wake Bukayo Saka, ameishia kusema tu 'ni Kama Messi'.

Arsenal iliibuka na ushini wa mabao 2-0 katika mchezo huo ambao Saka alipika bao moja na kufunga bao moja la ushindi baada ya lile la Kai Hevertz.

Arteta akizungumzia mchezo huo baada ya kumalizika alisema Saka kwa asilimia kubwa anafanana na staa wa zamani wa Barcelona na PSG, Lionel Messi kutokana na namna anavyocheza.

Saka alitoa asisti kwa Havertz aliyefunga bao la kwanza kipindi cha kwanza kabla kufunga bao la pili dakika ya 74.

Arteta alipoulizwa juu ya ubora wa Saka na inavyokuwa ngumu kwa mabeki kumzuia kutumia mguu wake wa kushoto alisema ni ngumu sana staa huyo kuzuiwa kutokana na ubora wake.

"Ukiwa na Lionel Messi kwenye timu, ndiye anaweza kufanya kama hivyo, lakini Saka amekuwa akifanya yeye na huwezi kabisa kumzuia, ni mchezaji bora sana kwenye timu hii," alisema Arteta.

Kocha huyo Mhispania pia aliwasifia wachezaji wake waliocheza michuano ya Euro ikiwamo Saka, Declan Rice na David Raya ambao hawakuwa sehemu ya kikosi katika maandalizi ya msimu.

Licha ya kutokuwa na timu pamoja wachezaji hao wameonyesha viwango bora kutokana na mazoezi binafsi waliyofanya.

"Sijashangazwa sana na kurudi kwao na kuonyesha kiwango bora licha ya kutofanya mazoezi na timu, hicho ndicho walichokuwa wanajiandaa nacho mara tu baada ya kumaliza mechi ya mwisho ya Euro, walinambia wanataka kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanakuwa sawa katika mchezo wa ufunguzi, nilizungumza nao baada ya mapumziko yao na niliwapa ratiba ya kufuata," alisema Arteta.

"Walitakiwa kurudi na kuingia katika timu mapema. Tayari walikuwa wakijiandaa walipokuwa likizo, ni moja ya vitu tunavyohitaji, ikiwa wachezaji wanajituma wenyewe ni rahisi kupandisha viwango vyao."

Kocha wa Wolves, Gary O'Neil alisema mbali ya kupoteza alifurahishwa na mchezo mgumu walioipa Arsenal.

"Nafikiri tulikuwa bora uwanjani na nilifurahishwa na kiwango chetu, ni wazi sipendi kupoteza mechi lakini nilifurahishwa jinsi tulivyoipa Arsenal mchezo mgumu. Tuliwawekea vikwazo na tukawafanya wapate nafasi chache. Hata tulipokuwa tunaongozwa 1-0, niliona sisi ndio tulikuwa na nafasi kubwa ya kupata ushindi kuliko wao, niseme walipata nafasi mbili wakazitumia na sisi tulipata kadhaa lakini hatukuzitumia."