Arteta kushusha wanne Arsenal
Muktasari:
- Arsenal kwa sasa inafikiria kumuuza Jakub Kiwior ili kupata nafasi ya kusajili kiungo mmoja kwa kutumia pesa itakazopata.
London, England. Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, bado hajamaliza, ndio. Mhispania huyu bado anahitaji wachezaji wasiopungua wanne kwa ajili ya kuboresha zaidi kikosi.
Arsenal kwa sasa inafikiria kumuuza Jakub Kiwior ili kupata nafasi ya kusajili kiungo mmoja kwa kutumia pesa itakazopata.
Kiwior, aliyejiunga na Arsenal akitokea Spezia mwaka 2023, amekuwa akiwindwa sana katika dirisha hili la majira ya kiangazi na timu kama Crystal Palace, FC Porto na vigogo kutoka Italia.
Arsenal imeweka wazi kwamba haihitaji kuuza ili kusajili wachezaji wengine kwa sababu pesa bado ipo na kanuni inawaruhusu lakini inaweza kufanya hivyo ikipokea ofa nzuri.
Katika wachezaji hao wanne, kwa mujibu wa Daily Mail, wawili kati ya wachezaji wanne beki na kiungo ambao wanatajwa kuwa ni Jon Martin(Real Sociedad) na Arnau Martinez(Girona).
Kwa upande wa wachezaji wawili waliobaki ni wale wa nafasi za mbele ambapo mmoja ni mchezaji wa Kimataifa wa Israel, Oscar Gloukh, mwenye umri wa miaka 21 ambaye tayari amecheza Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Red Bull Salzburg msimu uliopita kabla ya kutua Ajax katika dirisha hili la majira ya kiangazi.
Caleb Yirenkyi, 19, ni mchezaji mwingine ambaye anawindwa na tayari ameonyesha kiwango bora akiwa na FC Nordsjælland pia na timu ya taifa ya Ghana ambayo ameichezea kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Arsenal tayari imeshafanya usajili wa wachezaji kadhaa katika dirisha hili la majira ya kiangazi ikiwemo Viktor Gyokeres na Eberechi Eze.
Akizungumzia usajili wa Eze, Arteta alisema:"Tumemsaini mchezaji mwenye kipaji kikubwa na mwenye athari kubwa katika ligi hii, na zaidi ya hayo, ni mchezaji ambaye ana mapenzi na makubwa na klabu hii ya soka, ameonyesha hilo wazi, familia yake pia ina mapenzi, huitaji kutumia nguvu kuliona hilo. Nilikosa tukio la utambulisho lakini niliongea naye na alikuwa na tabasamu kubwa usoni."