Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asha Baraka amuangukia Dk Mwigulu akiomba uwanja wa Simba

Mbunge wa Viti Maalum, Asha Baraka wakati akichangia bungeni jijini Dodoma. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Asha ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 14,2026 alipokuwa akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu ambapo amemwomba kuiga mfano wa Waziri wa Habari na Michezo Paul Makonda aliyetoa ardhi kwa timu ya Yanga licha ya kuwa yeye ni shabiki wa Simba.

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Asha Baraka amemwomba Waziri Mkuu kuwasaidia Timu ya Simba ili nao wapate ardhi yao kama ilivyo kwa watani wao Yanga ambao tayari wamekabidhiwa hati ya umiliki.

Asha ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 14,2026 alipokuwa akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu ambapo amemwomba kuiga mfano wa Waziri wa Habari na Michezo, Paul Makonda aliyetoa ardhi ya kujenga uwanja kwa timu ya Yanga licha ya kuwa yeye ni shabiki wa Simba.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, vilabu vyetu vimekuwa vikicheza ligi na mashindano ya Kimataifa na kufanya vizuri kutokana na hamasa hasa ya goli na mama, leo nimemwona Waziri Makonda amekaa hapo, yeye akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa kiwanja kwa Klabu ya Yanga. Tunaomba na wewe ufanye hivyo kwa timu ya Simba,” amesema Asha.

Mbunge huyo amesema Klabu ya Simba imekuwa ikiomba Serikali kwa muda mrefu lakini haijafanikiwa hivyo akasema licha ya mapenzi ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba kwa timu ya Yanga, lakini afanye hivyo kwa Simba.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, fumba macho utupe uwanja na sisi Simba ili uweke kumbukumbu nzuri kwa Klabu yetu na mtupatie hati,” amesema Asha.

Mbunge huyo amesema siku za nyuma timu hizo zilikuwa zikifanya mazoezi yake katika maeneo ya Jangwani ambako sasa wenzao watahama baada ya kupata eneo lao maalumu huku Simba wakiwa na maombi bila mafanikio.

Juni 15, 2019, Makonda akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alitangaza kuipa Yanga ardhi eneo la Kigamboni ili ijenge uwanja kwa ajili ya matumizi yake.

Makonda alitangaza uamuzi huo katika Hafla Maalum ya kuichangia Yanga iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Machi 20, 2021, Makonda aliikabidhi Yanga cheti maalum cha kuthibitisha umiliki wa eneo hilo.