Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atimuliwa timu ya taifa Iran kisa picha na kiongozi wa Dubai

Mshambuliaji nyota wa Iran, Sardar Azmoun. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kwa sasa Azmoun anachezea klabu ya soka ya Shabab Al-Ahli ya Falme za Kiarabu. Amefunga mabao 57 katika mechi 91 za kimataifa kwa ajili ya nchi yake.

Mshambuliaji nyota wa Iran, Sardar Azmoun, amefukuzwa katika kikosi timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kukiuka kile kilichoonekana kuwa kitendo cha kutokuwa mwaminifu kwa serikali.

Vyombo vya habari vya Iran vinaripoti kwamba Azmoun, mwenye umri wa miaka 31, huenda asiichezee Iran katika Kombe la Dunia mwaka huu baada ya kushiriki picha (ambayo baadaye aliifuta) akipeana mkono na mtawala wa Dubai, Mohammed bin Rashid Al Maktoum.

Kwa sasa Azmoun anachezea klabu ya soka ya Shabab Al-Ahli ya Falme za Kiarabu.

Amefunga mabao 57 katika mechi 91 za kimataifa kwa nchi yake.

Ushiriki wa Iran katika Kombe la Dunia uko katika hali ya sintofahamu kutokana na mzozo unaoendelea na Marekani, Israel pamoja na washirika wao wa karibu katika Mashariki ya Kati ambapo Falme za Kiarabu ni mmoja wao.

Iran imeanzisha mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Falme za Kiarabu kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani na Israel, ambayo yalimuuwa Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei.

Baadaye mwanasoka huyo alifuta picha hizo kutoka kwenye mitandao yake ya kijamii, lakini alikosolewa kwenye televisheni ya serikali Alhamisi usiku, ambapo mchambuzi wa soka Mohammad Misaghi alielezea tabia ya mshambuliaji huyo kuwa ni kitendo cha kukosa uaminifu kwa taifa lake.

“Ni jambo la kusikitisha kwamba huna uelewa wa kutosha kujua ni aina gani ya tabia inayofaa kwa wakati fulani.

“Hatupaswi kulegeza maneno kwa watu wa aina hii. Wanapaswa kuambiwa kuwa hawastahili kuvaa jezi ya timu ya taifa.

“Hatuna uvumilivu kwa tabia ya kulalamika na utoto kama huu. Wachezaji wa timu ya taifa wanapaswa kuwa watu wanaoimba kwa fahari wimbo wa taifa na wanaostahili kuvaa jezi ya Iran,” amesema Misaghi.

Shirikisho la soka la Iran bado halijathibitisha taarifa kwamba Azmoun amefukuzwa kutoka timu ya taifa.

Awali alikuwa ameshiriki picha na kiongozi wa Dubai ambayo bado ipo kwenye akaunti yake ya Instagram tangu Januari 2025.

“Ilikuwa furaha na heshima kukutana na mmoja wa akili zilizofanikiwa zaidi duniani, Sheikh Mohammed bin Rashid,” aliandika kwenye maelezo ya picha hiyo. “Chagua klabu yako kwa makini.”

Azmoun amecheza maisha yake yote ya soka ya vilabu nje ya nchi, akiwahi kuchezea klabu za Zenit Saint Petersburg, Bayer Leverkusen na AS Roma, pamoja na kuiwakilisha Iran katika Kombe la Dunia la 2018 na 2022.

Ripoti isiyo na chanzo kutoka kituo cha habari cha Novad News ilisema Alhamisi kuwa amri ilitolewa ya kutaifisha mali za Azmoun, pamoja na mshambuliaji mwingine wa timu ya taifa anayekaa UAE, Mehdi Ghayedi, na mchezaji wa zamani wa kimataifa Soroush Rafiei.

Misaghi alikuwa akizungumza katika muktadha wa picha za hafla ya kuikaribisha timu ya taifa ya wanawake ya Iran kurejea Tehran baada ya kutoka Australia.

Wachezaji saba waliomba hifadhi nchini Australia baada ya timu hiyo kuitwa “wasaliti wa wakati wa vita” kwenye televisheni ya serikali ya Iran kwa kutokuimba wimbo wa taifa kabla ya mechi ya Kombe la Asia la Wanawake. Watano baadaye waliamua kurejea Iran.