Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea ilivyomnasa Garnacho Man United

Muktasari:

  • Inaelezwa kinachokwamisha dili lake ni kiasi cha fedha ambazo Man United inazitaka kuonekana nyingi kwa vigogo wa Chelsea.

London, England. Chelsea imeongeza jitihada kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Garnacho, 21, kutoka Manchester United dirisha hili.

Inaelezwa kinachokwamisha dili lake ni kiasi cha fedha ambazo Man United inazitaka kuonekana nyingi kwa vigogo wa Chelsea.

Taarifa zimefichua kwamba Mashetani Wekundu wanataka kiasi kisichopungua Euro 70 milioni ili kumuuza staa huyo ambaye kocha wa Ruben Amorim amempa ruhusa ya kuondoka kwani anaona haendani na mifumo yake. Hata hivyo, hiyo ni kinyume na jinsi kocha wa Chelsea, Enzo Maresca anavyofikiria kwani anamuona kuwa mmoja wa washambuliaji ambao watasaidia kuboresha kikosi chake na kuongeza namba ya mabao.

Staa huyo ameshafanya makubaliano binafsi na Chelsea na kinachosubiriwa ni makubaliano ya klabu na klabu ili dili likamilike.

Kwa sasa ana mkataba unaotarajiwa kumalizika Man United 2028.


Nicolas Jackson

ASTON Villa inapambana kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal, Nicolas Jackson, 24, kutoka Chelsea, lakini bei yake ya Pauni 60 milioni inadaiwa kuwa kikwazo. Jackson alijiunga na Chelsea Julai 2023 akitokea Villarreal kwa ada ya takriban Euro 37 milioni. Msimu wake wa kwanza alifunga mabao 17 katika mechi 44 za michuano yote. Mkataba wa staa huyo unatarajiwa kumalizika 2031.


Christopher Nkunku

BAYERN Munich ni kama imekwama kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, Christopher Nkunku, 27, jambo linalochelewesha lengo la Chelsea la kumsajili kiungo mshambuliaji wa Uholanzi Xavi Simons, 22, kutoka RB Leipzig. Mabosi wa Chelsea wanataka pesa watakayopokea kutokana na mauzo ya Nkunku kumsajili Simons. Mkataba unamalizika 2029.


Yoane Wissa

NEWCASTLE United haitaki kulipa zaidi ya Pauni 40 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Yoane Wissa, 28, katika dirisha hili. Dili hilo linaonekana kuwa karibu kufeli kwa sababu Brentford inahitaji takribani Pauni 60 milioni. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwakani.


Maghnes Akliouche

TOTTENHAM Hotspur imeelekeza macho kwa kiungo mshambuliaji wa Monaco, Maghnes Akliouche, 23,  anayeuzwa takribani Pauni 47.5 milioni. Mabosi wa Spurs wanamtaka kwa sababu ada yake ya uhamisho ni ndogo ikilinganishwa na ile ya winga Mbrazili Savinho ambaye Man City inahitaji Pauni 70 milioni. Msimu uliopita, Akliouche alihusika na mabao 13.


Tyler Dibling

CRYSTAL Palace inataka kumsajili winga wa Southampton, Tyler Dibling, 19, ili akachukue nafasi ya Eberechi Eze, 27, anayejiandaa kujiunga na Tottenham Hitspur dirisha hili. Dibling ambaye anachezea timu za vijana za England ameonyesha kuwa tayari kutua Palace, lakini timu hazijafikia mwafaka kwenye masuala ya ada ya uhamisho. Eze alifunga mabao 11 msimu uliopita na anadaiwa kuuzwa Pauni 60 milioni.


Douglas Luiz

KIUNGO wa Juventus na timu ya taifa ya Brazil, Douglas Luiz, anadaiwa kutarajiwa kujiunga na Nottingham Forest dirisha hili baada ya mmiliki wa Forest, Evangelos Marinakis, kufanya mazungumzo na kigogo wa Juventus, Damien Comolli na kufikia mwafaka. Luiz alijiunga na Juventus 2024 akitokea Aston Villa. Forest inamwona kama mbadala baada ya kupoteza baadhi ya mastaa.


Noah Okafor

LEEDS United iko tayari kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na timu ya taifa ya Uswisi, Noah Okafor, 25, katika dirisha hili kwa ada ya karibu Pauni 18.4 milioni. Okafor alijiunga na AC Milan akitokea RB Salzburg Julai 2023 kwa ada ya  Euro 14 milioni na msimu wake wa kwanza alifunga mabao manne na kutoa asisti mbili katika mechi 24 za Ligi Kuu Italia (Seria A). Ana mkataba na AC Milan hadi Juni 2028.