Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho anaswa akiendesha gari kinyume cha sheria

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Ingawa amepewa nafasi ya kujiunga na Al-Nassr ya Saudi Arabia, Garnacho ameripotiwa kukataa ofa hiyo na anapendelea kusalia kwenye Ligi Kuu ya England.

Manchester, England, Winga wa Manchester United, Alejandro Garnacho, ameibua tena mjadala baada ya kunaswa akiwasili Carrington kufanya mazoezi akiendesha gari aina ya Audi ambalo halijalipiwa kodi jambo linalomfanya avunje sheria za barabarani Uingereza.

New Content Item (1)

Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Serikali ya Uingereza, gari hilo la kifahari la Garnacho lilipaswa kulipiwa ushuru wa barabara tangu Oktoba Mosi 2024. Kisheria, magari yote yanayotumika au yaliyopo barabarani lazima yawe yamelipiwa kodi na kuwa na bima, vinginevyo mmiliki anaweza kutozwa faini au hata kushitakiwa mahakamani.

Kwa mujibu wa RAC, adhabu ya awali kwa kuendesha gari lisilolipiwa ni faini ya pauni 30 sawa na 100,000 shilingi za Kitanzania pamoja na asilimia 150 ya kiasi cha ushuru unaodaiwa. Endapo faini hiyo haitalipwa, mmiliki anaweza kushtakiwa mahakamani na kutozwa hadi pauni 1,000 (Sh3 milioni) au mara tano ya ushuru unaodaiwa.

Garnacho, ambaye bado hatima yake iko shakani chini ya kocha Ruben Amorim, amekuwa miongoni mwa wachezaji waliowekwa kando na klabu, wakijulikana kama orodha ya nyota ambao hawapo kwenye mipango ya kocha mpya.

Inadaiwa kuwa Garnacho aliwasili Carrington saa chache baada ya Amorim kuondoka, kama ilivyokuwa kwa Marcus Rashford wiki iliyopita. Garnacho aliungana na Rashford, Jadon Sancho, Antony na Tyrell Malacia kwenye kundi la wachezaji waliopatiwa muda zaidi kusaka timu nyingine kabla ya msimu mpya kuanza.

Hali ya Garnacho inaelezwa kuwa tata, huku klabu ikipendelea kumuuza kwenda klabu nyingine kwa sababu ya faida ya kifedha katika kanuni za Financial Fair Play. Ingawa amepewa nafasi ya kujiunga na Al-Nassr ya Saudi Arabia, Garnacho ameripotiwa kukataa ofa hiyo na anapendelea kusalia kwenye Ligi Kuu ya England.

Wakati huo huo, Rashford anahusishwa na uhamisho wa mkopo kwenda Barcelona, huku Sancho akiangaliwa na Juventus. Antony huenda kurejea Real Betis, naye Malacia ambaye amekuwa majeruhi muda mrefu, sasa anawindwa na Celtic ya Scotland.

Kwa sasa Garnacho na wenzake wameambiwa warejee Carrington wiki hii kwa mazoezi, huku wakifanya mazoezi mbali na kikosi cha kwanza cha Amorim ishara kwamba maisha yao Old Trafford huenda yakafika mwisho hivi karibuni.