Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Crawford amchapa Canelo Alvarez akitwaa mikanda mitatu ya dunia

Muktasari:

  • Terence Crawford anashikilia rekodi ya kuwa bondia pekee wa kizazi cha sasa kushikilia matatu matatu makubwa ya ngumi ya dunia kwa wakati mmoja.

Kinyume na matarajio ya wengi, bondia Terence Crawford amefanikiwa kuibuka mshindi wa pambano la ngumi dhidi ya Canelo ‘Saul’ Alvarez lililochezwa alfajiri ya kuamkia leo Jumapili, Septemba 14, 2025 huko Marekani.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 ameshinda kwa pointi pambano hilo lililofanyika Las Vegas baada ya kuonyesha kiwango bora katika raundi nyingi.

Jaji wa kwanza amempa Crawford ushindi wa pointi 116-112, Jaji wa pili akampa ushindi wa pointi 115-113 na Jaji wa tatu akampatia ushindi wa pointi 115-113.

Ushindi huo umemfanya Crawford kushinda mikanda ya ubingwa wa Dunia ya uzito wa kati ya WBC, WBO na IBF na mwenyewe amesema kuwa hajapata mafanikio hayo kibahati.

“Sipo hapa kwa kubahatisha,” amesema Crawford.

Pamoja na kupata ushindi huo, Crawford ameshindwa kusema kuwa ataastaafu ngumi au la baada ya ushindi huo ambao ni wa 42 mfululizo kwake kwenye ngumi.

“Sijui (kama nitastaafu). Nitakaa chini na timu yangu na tutazungumzia hilo,” amesema Crawford.

Kwa upande wake Alvarez amesema kuwa pamoja na kupoteza pambano hilo, anaona fahari kuwakilisha vyema nchi yake ya Mexico.

“Najisikia vizuri kushirikiana ulingo na wapiganaji wakubwa kama yeye. Kama tutafanya hivyo tena, litakuwa jambo jema.

“Alama yangu tayari iko pale na napenda kujitosa kwa sababu napenda masumbwi,” amesema Alvarez.

Hilo limekuwa pambano la tatu kwa Alvarez kupoteza katika ngumi za kulipwa kati ya mapambano 68 aliyopanda ulingoni