Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra, Aziz Ki mambo magumu Kombe la Dunia

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Mali inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi I la kuwania kufuzu Kombe la Dunia ikiwa na pointi nne kama ilivyo kwa Burkina Faso kwenye kundi A.

Dar es Salaam. Kupoteza mechi za jana dhidi ya Ghana na Misri, kumeziweka Burkina Faso na Mali ambazo ni timu za taifa za nyota wawili wa Yanga, Djigui Diarra na Stephane Aziz Ki katika nafasi ngumu kwenye harakati za kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Matokeo hayo yamefanya pengo la pointi kati yao na vinara wa makundi yao kuanza kuwa kubwa jambo linaloweka rehani ndoto za nyota hao wawili kushiriki Kombe la Dunia mwakani.

Kichapo cha mabao 2-1 ugenini mbele ya Misri, jijini Cairo jana, kiliifanya Burkina Faso ambayo anaichezea Aziz Ki kujikuta ipo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi A ikiwa na pointi nne.

Burkina Faso ambayo jana haikumchezesha Aziz Ki kwenye mechi hiyo iliyochezwa katika Uwanja wa kimataifa wa Cairo, imezidiwa kwa pointi tano na kinara Misri huku kila timu ikicheza mechi tatu na nafasi ya pili ipo Guinea Bissau yenye pointi tano.

Kwenye Uwanja wa Machi 26 jijini Bamako, wenyeji Mali walijikuta wakiduwazwa nyumbani na Ghana wakifungwa mabao 2-1.

Katika mchezo huo, Diarra hakupata nafasi ya kucheza na badala yake alitumika kipa Mamadou Samassa.

Ni ushindi ambao umeipeleka Ghana hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi I ikifikisha pointi sita sawa na kinara, Comoro.

Mali iliyo inashika nafasi ya tatu kwenye kundi hilo ikiwa na pointi nne sawa na Afrika ya Kati iliyopo nafasi ya nne.

Mambo yameonekana kwenda vizuri kwa kipa wa Azam FC, Mohamed Mustafa baada ya kuiongoza timu yake ya taifa ya Sudan kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Mauritania ambapo kipa huyo alicheza kwa dakika zote 90.

Ushindi umeifanya Sudan kuongoza kundi B ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Senegal iliyo na pointi tano na DR Congo iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne.

Makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 yako tisa na timu itakayomaliza ikiwa kileleni mwa msimamo itafuzu moja kwa moja fainali hizo.

Pia kutakuwa na Afrika kupata nafasi ya 10 kupitia mechi za mchujo dhidi ya timu za mabara mengine.