Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

England waandaa paredi ya ubingwa kimya kimya

Muktasari:

  • Maafisa waandamizi wanaripotiwa kufanya mashauriano yasiyo rasmi na FA kuhusu namna bora ya kudhibiti umati unaokadiriwa kufikia mamilioni ya watu.

Imefichuka kuwa Serikali ya England inaandaa kwa siri mipango ya kufanya paredi kubwa litakalogharimu Pauni 500,000 iwapo timu ya taifa ya nchi hiyo itatwaa Kombe la Dunia.

Watumishi wa umma wamepewa jukumu la kuandaa sherehe za kitaifa kwa kuzingatia uwezekano wa kikosi cha kocha Thomas Tuchel kufika mbali na kutwaa ubingwa msimu huu wa kiangazi.

Mipango inaendelea kwa ajili ya moja ya maandamano makubwa zaidi ya ushindi kuwahi kufanyika England, yakitarajiwa kufanyika jijini London katika wiki itakayofuata baada ya mechi ya fainali, Julai 19.

Wizara ya Masuala ya Kidijitali, Utamaduni, Vyombo vya Habari na Michezo (DCMS) inaandaa tarehe maalumu ndani ya siku chache baada ya fainali hiyo.

Hatua hii inafuatia maandalizi ya haraka yaliyofanywa na Serikali pamoja na Chama cha Soka England (FA) kwa ajili ya gwaride la timu ya wanawake ya England, maarufu kama Lionesses, baada ya kutetea ubingwa wao wa Euro mwaka 2025.

Maafisa waandamizi wanaripotiwa kufanya mashauriano yasiyo rasmi na FA kuhusu namna bora ya kudhibiti umati unaokadiriwa kufikia mamilioni ya watu.

Kuandaa mipango hiyo pekee tayari kumetumia kiasi kikubwa cha fedha, huku maafisa wakiwa katika hatua za kukodisha basi la ghorofa mbili kwa ajili ya paredi, jukwaa kubwa na burudani za moja kwa moja.

Hata hivyo, gharama hiyo inaonekana kuwa ya thamani kutokana na matarajio ya kuongeza ari na morali ya taifa iwapo England itashinda Kombe la Dunia.