Fei Toto, Yanga kimeeleweka asubiri kutambulishwa

Dar es Salaam. Taarifa za chini chini zilizotufikia Mwananchi linajua kabla ya jua kuzama leo Jumatano, Feisal Salum 'Fei Toto' atatambulishwa rasmi ndani ya Azam.

Licha ya Azam kufanya siri, lakini Mwananchii linajua klabu hiyo ilimalizana na Yanga jana jijini Dar es Salaam  baada ya kikao kizito cha pande zote mbili.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwaomba Yanga kumaliza mgogoro na kiungo huyo Mzanzibari, ili mambo mengine yaendelea.

Fei aliingia kwenye mgogoro huo, baada ya kuvunja mkataba bila kuzingatia kanuni, hadi kesi kupelekwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) bado Yanga ikawa kwenye upande wa haki.


Kwa habari zaidi endelea kufuatilia kwenye mitandao yetu na Gazeti la Mwananchi kesho Alhamisi.