Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gofu ndani ya hifadhi ya Serengeti kivutio kipya

Mara. Ni kama simulizi yenye kusisimua ambapo wachezaji wa gofu watakuwa wakikutana nao pale watakapokuwa wakicheza huku kando wakishuhudia wingi wa wanyama na ndege zikitua.

Wanyama kama pundamilia, swala, nyumbu, tembo na au twiga watakuwa wakipita kando au karibu na Uwanja wa gofu unaojulikana ‘Serengeti National Park Golf Course’ ambao unajengwa eneo la Fort Ikoma, nje kidogo ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) kwa thamani ya zaidi ya Sh9.5 bilioni, utakuwa na viwanja 18 wenye hadhi ya kimataifa.

Mbali na mandhari ya kuvutia, uwanja huo unazingatia viwango vya juu vya ubora katika usanifu na ujenzi. Unajengwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa na vifaa bora, ukijumuisha njia za kuchezea zilizopangwa kwa ufanisi, maeneo ya kupumzika ya kisasa, na miundombinu rafiki kwa mazingira.

Eneo lake la kimkakati, likiwa karibu na uwanja mdogo wa ndege, linarahisisha upatikanaji kwa wageni wa ndani na wa kimataifa. Hii inaufanya kuwa kivutio kipya cha utalii na michezo, chenye uwezo wa kuchochea uchumi wa kanda na kuvutia mashindano ya kimataifa ya gofu.

Mwananchi limefika katika mradi huo wiki iliyopita na kukuta shughuli za ujenzi zikiendelea na kupata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wasimamizi wa ujenzi Zacharia Edward ambaye anasema wamekwisha kamilisha viwanja 15 kati ya 18 yenye changamoto tofauti, na urefu wa kilomita 7.05.

“Huu uwanja utakuwa na hadhi ya kimataifa pindi utakapokamilika. Utakuwa moja ya viwanja bora na vya kipekee kwani mtu atakuwa akicheza huku wanyama wakiwa pembezoni,” anasema Edward.

Akijibu swali aliloulizwa wanyama hao hawatakuwa na madhara amesema, eneo walipojenga hakutakuwa na wanyama wakali akiwataja kwa uchache nyumbu, pundamilia, twiga na swala.

Upekee mwingine wa uwanja huo, Edward anasema pembeni yake kuna uwanja mdogo wa ndege: “Kwa hiyo watalii, wafanyabiashara na wana michezo wakishuka tu wanaingia uwanjani.”

Aidha, Edward ambaye ni mchezaji wa gofu amesema kiwanja hicho kitakuwa cha pili kwa ubora wa kimataifa na hata mvua kubwa zikinyesha kinatengenezwa kukiwezesha dakika chache baada ya kunyesha maji yote yanaotoka na mchezo kuendelea.

Amesema pindi utakapokamilika, uwanja huu wa kipekee utapambwa na mandhari ya kuvutia yenye wanyamapori wanaozunguka, hivyo kuongeza mvuto wa kipekee kwa wapenzi wa gofu na watalii.


Umefikia asilimia 65

Dk Richard Matolo ambaye ni mmoja wa wahandisi wanaosimamia ujenzi huo anasema ujenzi umefikia asilimia 65 ukitekelezwa katika eneo la hekta 450 ndani ya hifadhi, likiwa limebuniwa kwa viwango vya kimataifa.

“Mashimo yamepangwa kwa ustadi wa hali ya juu, tukizingatia ukubwa wa eneo. Hii inampa mchezaji uzoefu wa aina tofauti na kuongeza mvuto wa kimataifa,” anasema Dk Matolo.

Anasema gharama ya mradi huo inakadiriwa kufikia Sh 9.5 bilioni hadi kukamilika kwake, na kwamba mbali na uwanja wa golf, kutajengwa pia luxury sleeping cottages kwa ajili ya wageni, ili kuongeza thamani ya utalii na kuliingizia Taifa mapato zaidi.

“Tayari tumeanza kuwaalika wawekezaji kuja kushiriki kwenye sehemu mbalimbali za huduma ndani ya mradi huu,” anasema.

Mradi huu unatarajiwa kuvutia si tu watalii wa kawaida bali pia wachezaji wa golf kutoka pande mbalimbali za dunia, na hivyo kuiweka Serengeti katika ramani ya kimataifa ya michezo na utalii wa hadhi ya juu.

Naye Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Alex Choya anasema:"Mchezo huu itakuwa sehemu ya zao la utalii, kuongeza watalii lakini itakuwa chanzo cha ongezeko la mapato."

Choya anasema hiyo ni miongoni mwa mikakati mbalimbali ya kuendelea kuifanya hifadhi hiyo kuwa bora ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Mei 9, 2025, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbasi alitembelea kujionea maendeleo yake ambapo anasema ukikamilika: “Unafungua zao jingine muhimu la kimkakati kwetu, ambalo ni utalii wa michezo. Nimewaagiza Tanapa kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa haraka.”

Dk Abbas amesema uwanja huo utakuwa kichocheo cha maendeleo ya viwanja vingine vya michezo katika eneo hilo, kwa lengo la kuendeleza zao la utalii wa michezo ambalo lina mchango mkubwa kiuchumi na kitega uchumi kipya kwa mbuga za wanyama na jamii zinazozizunguka.


Wasemacho wadau

Mmoja wa waongoza watalii, Peter Lyimo anasema hatua inayofuata kwao baada ya ujenzi kukamilika ni kuanza kuuza zao hilo kwa watalii na ana amini litapokelewa vizuri.

"Fikiria yaani unacheza gofu huku unashuhudia wanyama, ni utalii wa aina yake. Tunashukuru kwa aliyebuni wazo hili," anasema Lyimo.

Paul Myers, mtalii kutoka Marekani aliyekuwa hifadhini anasema hicho kinaweza kuwa sababu ya yeye siku za usoni kutamani kurudi Tanzania kucheza gofu hifadhini.

Anasema ametembelea mbuga ya Serengeti:"Hakika ni nzuri na inavutia, unaona wanyama wa aina zote kwa ukaribu kabisa, nimefurahi sana. Hilo la Gofu nitarudi kucheza.