Golikipa wa Mamelodi aweka historia Afrika

Muktasari:
- Williams anaweka historia kuwa golikipa wa kwanza anayechezea klabu ya Afrika kujumuishwa kwenye orodha ya tuzo ya Ballon d’Or ya golikipa bora wa mwaka
PRETORIA,SOUTH AFRICA. Mlinda mlango wa Mamelodi na timu ya Taifa ya Afrika Kusini Ronwen Williams ameweka historia ya golikipa wa kwanza anayechezea klabu ya Africa kutajwa kwenye orodha ya magolikipa wanaoshindania tuzo ya Ballon d’Or ya golikipa bora wa mwaka.
Magolikipa wengine wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na Gianluigi Donnarumma, Unai Simon, Giorgi Mamardachvili, Diogo Costa, Gregor Kobel, Mike Maignan, Andrei Lounine, Yann Sommer, Emiliano Martinez na Ronwen Williams.
Williams alichaguliwa kuwa golikipa bora kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 iliyofanyika Ivory Coast baada ya kucheza mechi nne bila kuruhusu bao na kuiongoza Afrika Kusini kumaliza nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo.

Msimu uliyopita kwenye michezo 59 aliyocheza Williams ni michezo 35 ambayo hakuruhusu nyavu zake kutikiswa ‘Cleen sheets’ huku akiiongoza Mamelodi Sundowns kuchukua ubigwa wa African Football League pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Africa Kusini.
Ni mchezaji mmoja tu kutoka Bara la Afrika ambaye aliwahi kuchukua tuzo ya Ballon d’Or naye ni George Weah Raisi wa sasa wa Liberia na nyota wa zamani wa Arsenal, PSG na AC Milan alipofanya hivyo mwaka 1995.