Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola ampiga chini Grealish

Muktasari:

  • Bosi huyo wa Manchester City, Guardiola alionekana kuwa na hasira kwamba hafurahishwi na Grealish.

MANCHESTER, ENGLAND: Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amempiga chini Jack Grealish kwenye kikosi chake kilichocheza mechi ya mwisho msimu huu, kisha akisema winga huyo Mwingereza anaweza kuondoka mwisho wa msimu.

Bosi huyo wa Manchester City, Guardiola alionekana kuwa na hasira kwamba hafurahishwi na Grealish.

Kocha huyo Mhispaniola alisema uamuzi wa kumwaacha Grealish lilikuwa ni jambo la kawaida tu katika kukibadili kikosi chake. Lakini, Guardiola alituma ujumbe wa wazi kabisa kwa staa huyo aliyesajiliwa kwa ada ya Pauni 100 milioni, Agosti mwaka 2021 kwamba hajali kitu.

Alisema: “Kunakuwa na wachezaji watano au sita nawaacha kwenye kikosi kila wiki. Na sasa umefika uamuzi huu, mimi ndiye niliamua. Sawa, Jack lazima acheze. Huo ndio ukweli.”

Lakini, alipoulizwa kama hakuwa na furaha na Grealish, Guardiola alijibu kwa hasira, akisema: “Usiniulize kuhusu Jack. Nani amesema simfurahii Jack? Rico (Lewis) sikumchagua pia, (James) McAtee naye alikosa mechi za Aston Villa na Wolves kwanini hamniulizi McAtee? Haya si mambo binafsi.

“Nina wachezaji 24, lazima niwaweke kando wachezaji sita au watano kwenye kila mechi. Namchukulia Jack kama ninavyowachukulia wachezaji wengine (Abdukodir) Khusanov, McAtee na wote.”

Guardiola alisema kwamba kumaliza namba tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ni kama kushinda ubingwa kwa msimu huu. Alisema amefurahi kikosi hicho kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya mwanzoni kuwa na wasiwasi kwamba wasingeweza kufanya hivyo baada ya kupoteza dhidi ya Arsenal na Liverpool mwanzoni mwa mwaka huu.

Lakini, alikoshwa na namna wachezaji wake walivyopambana kuanzia Machi mwaka huu, wakicheza mechi 11 bila ya kupoteza kwenye Ligi Kuu England.

Guardiola alisema: “Nimepata nafuu. Kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kama kubeba ubingwa kwa upande wetu.”