Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gwiji wa Liverpool afariki Dunia

Muktasari:

  • Jones ataendelea kukumbukwa kama mmoja wa wachezaji walioweka alama ya kudumu si tu kwa Liverpool na Wrexham, bali kwa soka la England kwa ujumla.

Beki wa zamani wa Liverpool, Joey Jones, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70. Jones, ambaye aliingia kwenye vitabu vya historia kwa kushinda mataji mawili ya European Cup akiwa na Liverpool katika miaka ya 1970, ameacha pengo kubwa katika soka la England na Wales.

Joey, aliyekuwa pia kipenzi kikubwa cha mashabiki wa Wrexham alikodumu kwa vipindi vitatu tofauti alijulikana kama Mr Wrexham kutokana na mchango wake mkubwa kwa klabu hiyo. Pia aliwahi kuichezea Chelsea na Huddersfield, huku akicheza mechi 72 za kimataifa na timu ya taifa ya Wales mwaka 1975 hadi 1982.

Mchezaji mwenzake wa zamani Liverpool, John Aldridge, aliongoza salamu za rambirambi kwa kuandika kwenye X (zamani Twitter):

"Habari nyingine ya kusikitisha, Joey Jones amefariki usiku wa kuamkia leo. Alikuwa mtu wa kipekee, beki aliyecheza kwa moyo wote kwa klabu zote alizowahi kuzitumikia. Nawapa pole familia yake. Nilikuwa na bahati kubwa kukutana naye mara nyingi. RIP shujaa wetu.”

Jamie Carragher, beki wa zamani wa Liverpool, naye ametoa heshima zake fupi: "RIP Joey Jones."

Safari ya mafanikio Liverpool

Jones alijiunga na Wrexham akiwa kijana mwaka 1971 na kushinda Kombe la Wales mwaka 1975. Mwaka huohuo alijiunga na Liverpool ambapo alishinda European Cup mara mbili (1977 na 1978), pamoja na ubingwa wa First Division 1976-77, UEFA Cup, na European Super Cup.

Liverpool ilitoa taarifa rasmi ikieleza huzuni kubwa kufuatia kifo cha mchezaji wao wa zamani, ikihitimisha kwa kusema:

"Mawazo ya kila mtu ndani ya LFC yako pamoja na familia na marafiki wa Joey katika kipindi hiki kigumu."

Jones alirejea Wrexham mwaka 1978 kama mchezaji ghali zaidi wa klabu hiyo kwa ada ya pauni 200,000. Baada ya miaka minne, alienda Chelsea na kusaidia kuokoa klabu hiyo kushuka daraja kabla ya kuipandisha Ligi Kuu msimu uliofuata. Mwaka 1985 alijiunga na Huddersfield na kuteuliwa mchezaji bora wa mwaka kabla ya kurudi tena Wrexham kwa mara ya mwisho.

Wrexham wamethibitisha kuwa wanapanga kumuenzi gwiji huyo kwa kuweka sanamu yake katika uwanja wao wa mpira.

Jones ataendelea kukumbukwa kama mmoja wa wachezaji walioweka alama ya kudumu si tu kwa Liverpool na Wrexham, bali kwa soka la England kwa ujumla.