Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hakimi aitwa mahakamani, aituliza Morocco

Nahodha wa Morocco, Achraf Hakimi. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Morocco imeanza fainali za Kombe la Dunia kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Brazil na kesho Jumamosi itakabiliana na Scotland.

Nahodha wa Morocco, Achraf Hakimi ameishusha presha timu yake ya taifa, saa chache kabla ya kuivaa Scotland baada ya kusema kuwa uamuzi wa mahakama ya Ufaransa kuhusu tuhuma zake za kubaka haumpi wasiwasi na haumtoi mchezoni.

Kauli hiyo ya Hakimi imekuja muda mfupi baada ya rufaa yake ya kuomba shauri hilo juu ya tuhuma zake za kubaka zitupiliwe mbali.

Taarifa hizo zilihofiwa kwamba zingeweza kuharibu utulivu wa kambi ya Morocco inayojiandaa na mechi hiyo ya pili dhidi ya Scotland lakini Hakimi amewataka wenzake wawe na utulivu.

“Stori ambazo si zangu zinazungumzwa kwa gharama ya maisha yangu na familia yangu… nimekuwa nikisubiri kusimama mbele ya mahakama na sasa niko tayari kujitetea,” amenukuliwa akisema.

Hakimi amesema kuwa kwa muda mrefu ameamua kukaa kimya ili kutoa fursa kwa mamlaka za kisheria kuendelea na uchunguzi juu ya suala hilo.

Tuhuma hizo kwa Hakimi zilianza Machi 2023 ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 24 alipomtuhumu beki huyo kuwa alimbaka nyumbani kwake, jijini Paris.

Hata hivyo Hakimi ameonekana kukanusha hilo na amesema kuwa yuko tayari kujitetea kwa vile hakuwahi kufanya jambo hilo.