Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatima Uchaguzi TFF mahakamani Aprili 16

Muktasari:

“Nimeridhika kuahirishwa kwa kesi na naahidi kukamilisha maelezo ya madai siku ya Jumatatu tarehe 4 mwezi ujao,”

HATIMA ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania sasa itajulikana  Aprili 16, wakati Mahakama Kuu ya Mwanza itakapotoa hukumu ya kesi ya Richard Rutambura aliyepinga kufanyika kwa uchaguzi huo.

Mwanzoni mwa wiki hii, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilisoma kwa mara ya kwanza kesi iliyofunguliwa na Rutambura kupinga kufa nyika kwa uchaguzi waa TFF kutokana na kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 11 baada ya mahakama kukosa vielelezo muhimu vya madai ya Rukambura na hivyo kumwamuru mlalamikaji kukamilisha maelezo ya madai yake na kuyawasilisha mahakamani hapo kabla ya kutoa hukumu yake hapo Aprili 16 mwaka huu.

Akizungumzia kuahirishwa kwa kesi yake na kutakiwa kukamilisha madai yake kwa maandishi, Rukambura alisema hana shaka na uamuzi wa mahakama kwani yeye ameridhika na uchaguzi huo kusitishwa ili haki juu ya madai yake itendeke.
“Nimeridhika kuahirishwa kwa kesi na naahidi kukamilisha maelezo ya madai siku ya Jumatatu tarehe 4 mwezi ujao,” alisema.

Rukambura aliondolewa katika mchakato wa uchaguzi wa TFF kwa madai ya kuvunja kanuni za uchaguzi ya shirikisho hilo kwa kuomba nafasi mbili za uongozi, urais na ujumbe wa kamati ya utendaji.

Akizungumzia sakata hiyo, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema hawawezi kusema lolote ila kikao cha Kamati ya Utendaji kitachokutana Jumamosi hii ndicho kitakachoweza kutoa kauli.

Hata hivyo, Osiah alisema pamoja na kamati hiyo kukutana kujadili kauli ya Waziri Fenella Mukangara, bado hawatakuwa uamuzi wowote katika suala la uchaguzi mpaka hapo kesi iliyofunguliwa Mwanza imalizike.

Alisema mambo ya kesi yanazuia uchaguzi kufanyika hivyo hatima ya yote hayo ni mpaka kesi hiyo kumalizika ndipo watakuwa na kauli kuhusiana na uchaguzi wao.

“Kama mnavyojua kukiwa na kesi kama hiyo ina maana shughuli zote za uchaguzi zinasimama na hata kikao tu takachokaa Jumamosi hatuwezi kuzungumzia mambo ya uchaguzi zaidi ya kujadili kauli ya Waziri tu,” alisema Osiah.

Kwa mujibu wa Sheria za Fifa ibara ya 64, kifungu cha pili na tatu kinasema ni marufuku masuala ya michezo kwenda kusikilizwa kwenye mahakama za kawaida labda kwa ruhusa maalumu ya Fifa.
Osiah alisema licha ya Fifa kukataza mambo ya soka kwe nda mahakamani, lakini wao wenyewe ndiyo watatolea ufafanuzi mara baada ya kuwasili nchini mwezi ujao.

“Siwezi kuwajibia Fifa kutokana na uchaguzi kupelekwa mahakamani, hayo watakuja kuyamaliza watakapofika na kujionea hali halisi kabla ya kusema nini kiendelee,” aliongeza.