Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hersi:Tumegomea bilioni 5 kumuuza Mzize

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said, amefichua kwamba wakati wa presha kubwa ya kutakiwa kuuzwa kwa mshambuliaji wao Clement Mzize, klabu hiyo ilipokea ofa ya ya dola 2 milioni.

Hersi ametangaza hilo kwenye mkutano mkuu unaoendelea, akisema ofa ya mwisho ambayo ilikuja kwenye klabu hiyo ilikuwa Dola 2 Milioni (sh 5 Bilioni).

Hersi alisema hata hivyo uongozi wao ulizuia kumuuza, akisema isingekuwa rahisi kufanya biashara hiyo kwa kuwa bado Yanga ilikuwa inahitaji nguvu ya mshambuliaji.

"Ofa zilikuwa nyingi sana kwa kijana wetu lakini Yanga haikuwa na nia mbaya tulikuwa tunajua tunachokitaka," amesema Hersi.

"Wakati wa presha wa hizo ofa, Mzize alinipigia simu akaniuliza rais wangu niambie msimamo wa klabu ni upi, unataka niende au nisiende.

"Nikamwambia Mzize, tulia kwasasa piga kazi na timu ya taifa endelea kukiwasha piga mabao, ukimaliza CHAN tutazungumza.

Aidha Hersi akasema baada ya fainali hizo Mzize akaboreshewa maslahi na kuwa mchezaji anayelipwa vizuri ndani ya klabu hiyo.

"Hivi tunavyozungumza, Mzize amebakiza miaka miwili alimaliza mwaka mmoja ujao hapo ndio tutaangalia namna ya kumuuza.