Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hili hapa jeshi la Gamondi AFCON 20205, mastaa kibao wakifyekwa

Muktasari:

  • Katika Fainali za AFCON 2025 zitakazofanyika Morocco, Tanzania imepangwa kundi C na timu za Uganda, Tunisia na Nigeria.

Dar es Salaam. Kikosi cha mwisho cha wachezaji 28 wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitakachoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kuanzia Desemba 21, mwaka huu kimewekwa hadharani.

Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi amepunguza wachezaji 27 kutoka katika kikosi cha awali kilichokuwa na wachezaji 55.

Idadi kubwa ya wachezaji waliopunguzwa ni wale wanaocheza katika klabu zinazoshiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Uamuzi wa kushtukiza katika uteuzi wa kikosi hicho cha mwisho unaweza kuwa ule wa kuachwa kwa kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya.

Mshambuliaji wa Simba, Selemani Mwalimu, naye hatokuwemo katika fainali za AFCON 2025 kama ilivyo kwa nyota wa Yanga, Offen Chikola.

Licha ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo dhidi ya Simba ambao aliibuka Mchezaji Bora wa mechi, mshambuliaji Nassor Saadun wa Azam sio miongoni mwa nyota ambao Gamondi amechagua kwenda nao Morocco.

Kazi nzuri iliyofanywa na nyota wa JKT Tanzania ya kupachika mabao matano yaliyomfanya awe kinara wa Ufungaji katika Ligi Kuu Tanzania Bara hadi sasa, hakijatosha kumshawishi Gamondi kumuingiza katika kikosi chake cha mwisho  kwa ajili ya AFCON.

Nahodha Mbwana Samatta anayecheza Le Havre ya Ufaransa, ataongoza kundi la wachezaji watakaopeperusha bendera ya Tanzania huko Morocco huku jina la Saimon Msuva anayecheza Al Talaba ya Iraq nalo likiwa kundini.

Wachezaji 28 wanaounda kikosi cha mwisho cha Taifa Stars kwa ajili ya AFCON 2025 ni Yakoub Suleiman, Hussein Masalanga, Zubeir Foba, Shomari Kapombe, Bakari Mwamnyeto, Lusajo Mwaikenda, Mohamed Hussein, Nickson Kibabage na Alphonce Mabula.

Pia kuna Wilson Nangu, Novatus Dismas, Morice Abraham, Yusuph Kagoma, Kelvin Nashoni, Haji Mnoga, Ibrahim Abdullah, Dickson Job, Habibu Iddi, Tarryn Allarakhia na Charles M’mombwa.

Wengine ni Pascal Msindo, Feisal Salum, Abdul Suleiman, Idd Selemani, Kibu Denis, Mbwana Samatta, Kelvin John na Saimon Msuva.

Katika Fainali za AFCON 2025, Taifa Stars ipo kundi C lenye timu za Tunisia, Uganda na Nigeria.

Desemba 23, 2025, Taifa Stars itafungua na Nigeria kisha Desemba 27, 2025 itacheza na Uganda na mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Tunisia itakuwa Desemba 30, 2025.