Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ijue Hoteli ya kifahari itakayotumiwa na Taifa Stars Morocco

Muktasari:

  • Katika Fainali za AFCON 2026, Taifa Stars itacheza mechi zake mbili za kwanza za hatua ya makundi dhidi ya Nigeria na Uganda katika Jiji la FEZ na mechi ya mwisho dhidi ya Tunisia itakuwa Rabat.

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepangiwa katika Hoteli ya Kifahari ya Le tour Hassan Palace iliyopo jijini Rabat, pindi itakapofika Morocco kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

Hoteli hiyo ilijengwa mwaka 1912 na hadi sasa imebakia kuwa miongoni mwa hoteli za muda mrefu zinazotambulisha utamaduni wa Morocco.

Kutokana na usanifu uliotumika katika ujenzi wake na mazingira ya kuvutia, Hoteli hiyo imekuwa ikitumika kuandaa matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa nchini Morocco.

Kuna vyumba vya aina tano tofauti katika Hoteli hiyo ambapo kila aina ina gharama zake.

Gharama ya chini kabisa ya chumba kwa siku katika Hoteli hiyo ni Dirham 2660 za Morocco (Sh714832).

Kuna migahawa sita ndani ya Hoteli hiyo inayotoa huduma ya vyakula vyenye ladha ya Kimorocco na pia ladha za maeneo mengine tofauti duniani.

Ipo katikati ya Jiji la Rabat na ina huduma zote muhimu na za kisasa kama vile mabwawa ya kuogelea, masaji na SPA na ipo Umbali wa Kilomita nane kutoka Uwanja wa Ndege wa Rabat.

Katika Fainali za AFCON 2026, Taifa Stars itacheza mechi zake mbili za kwanza za hatua ya makundi dhidi ya Nigeria na Uganda katika Jiji la FEZ na mechi ya mwisho dhidi ya Tunisia itakuwa Rabat.

Umbali wa Rabat hadi FEZ kwa basi unakadiriwa kuwa Kilomita takribani 200.