Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kevin Keegan afariki dunia, chanzo chatajwa

Muktasari:

  • Baada ya kustaafu kucheza, Keegan alijikita kwenye ukocha, akizinoa Newcastle United, Fulham, timu ya taifa ya England na Manchester City.

London, England. Nyota wa zamani wa Liverpool, Newcastle United na timu ya taifa ya England, Kevin Keegan, amefariki dunia leo Jumatatu, Julai 20, 2026 akiwa na umri wa miaka 75.

Keegan amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa saratani ya tumbo, ambao Machi mwaka huu ulibainika kuwa umefikia hatua ya nne.

Taarifa iliyotolewa na familia yake imesema kifo cha Keegan kimeacha pengo kubwa, huku ikieleza kuwa nyakati zake za mwisho alikuwa amezungukwa na mke wake pamoja na watoto wake.

“Ni kwa huzuni kubwa sana tunatangaza kwamba Kevin Keegan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75.

“Aliyekuwa mchezaji na kocha wa timu ya taifa ya England alikuwa akipambana na ugonjwa wa saratani, na katika dakika zake za mwisho alikuwa amezungukwa na mke wake pamoja na binti zake.

“Kevin, mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mara mbili, alikuwa mume, baba na babu aliyependwa sana. Familia inapenda kuwashukuru madaktari na timu yote ya wataalamu wa afya waliomhudumia Kevin kwa msaada wao mkubwa,” ilisema taarifa hiyo.

Familia yake imeomba faragha katika kipindi hiki kigumu.

Keegan, ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliowahi kupata mafanikio makubwa katika soka la England, alichezea klabu sita tofauti na kufunga mabao 204 katika michezo 592.

Kati ya klabu hizo, Liverpool na Newcastle United ndizo zilizompa umaarufu mkubwa, huku pia akiichezea England mara 63.

Akiwa Liverpool, Keegan alishinda mataji mbalimbali ikiwemo Ligi ya England na Kombe la Ulaya kabla ya kuhamia Hamburg ya Ujerumani, ambako aliendelea kung'ara na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya (Ballon d'Or) mara mbili.

Baada ya kustaafu kucheza, Keegan alijikita kwenye ukocha, akizinoa Newcastle United, Fulham, timu ya taifa ya England na Manchester City.

Newcastle United imesema imesikitishwa na kifo cha Keegan, ikimtaja kuwa mmoja wa watu waliokuwa na ushawishi mkubwa katika historia ya klabu hiyo.

“Kevin alikuwa zaidi ya mchezaji na kocha wa hadhi ya kipekee. Alikuwa moyo uliokuwa ukiipa uhai Newcastle United kwa vizazi vingi vya mashabiki.

“Akiwa mchezaji, alionyesha kipaji cha kiwango cha dunia, ari ya mafanikio na imani katika Uwanja wa St James’ Park. Akiwa kocha, aliamsha upya matumaini ya jiji letu na kuwapa mashabiki fahari,” ilisema klabu hiyo.

Keegan ataendelea kukumbukwa kama mmoja wa mastaa wakubwa wa soka la England, akiwa na historia ya mafanikio ndani na nje ya uwanja.