Kiduku ashinda kwa pointi, ashindwa kuvunja rekodi ya Mzungu

Twaha Kassim 'Kiduku' ameshinda kwa pointi za majaji wote dhidi ya Iago Kiziria usiku huu mjini Morogoro.

Bondia huyo ametawazwa kuwa bingwa wa mabara wa UBO na PST baada ya kumaliza raundi zote 10 japo ameshindwa kuvunja rekodi ya mpinzani wake, ambaye hilo ni pambano la 10 kupoteza, lakini hajawahi kupigwa kwa KO wala TKO.

Majaji wawili walitoa pointi 98-92  kwa Kiduku na mmoja pointi 97-93 kwa bondia huyo aliyekuwa akicheza nyumbani kwenye ardhi ya Morogoro